Na Penina Malundo, timesmajira
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania (JMAT),Sheikh Alhad Mussa Salum amesema Jumuiya yao haitakubali kuona mtu yoyote anachezea amani ya nchi na wao wakamuangalia kwani Jumuiya ipo kwaajili ya kusaidia Serikali katika kudumisha amani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maonyesho ya 47 ya Biashara Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere alisema JMAT ni muunganiko wa muunganiko wa viongozi wa dini hivyo hawawezi kukubali amani ya nchi ikatoweka.
Alhad Mussa amesema lengo kubwa la wao kushiriki katika maonesho hayo ya Sabasaba ni kuleta biashara yao kubwa katika ya kuuza amani ya nchi kwa Watanzania.
“Wakati tunajianda katika banda letu kuna majirani wetu hawa wachina na wengine wageni walikuwa wanatushangaa kuona banda letu limejaa biblia na misaafu wanatuuliza sisi tunapata faida gani,”amehoji na kusema
“Tuliwajibu na kuwaambia sisi biashara yetu ni amani na utulivu ndicho ambacho tunauza humu Sabasaba. Amani na utulivu umewafanya wao kufanya biashara sisi biashara yetu haina faida. Faida yetu ni kuona Tanzania inabaki kuwa salama na kuwa na mahusiano mazuri kati ya wana dini ,”amesema.
Alidha amesema biashara ya kuwauzia Watanzania amani waone thamani yake imewafanya waonekani wapo tofauti na mabanda mengine.
“Mabanda yote yapo kibiashara zaidi lakini sisi tumejikita kuuza amani na utulivu. Tunawauzia Watanzania tunawaambia wanunue hii amani wachague amani na utulivu katika nchi yetu ndio maana tupo hapa watu wa madhehebu mbalimbali tunapigania mahusiano haya,”amesema Sheikh Salum.
Amesema anaipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) kwa namna walivyojipanga katika maonyesho ya mwaka huu yamekuwa ni mazuri na viongozi wengi wametembelea mabanda kujionea bidhaa mbalimbali.
“Watanzania tupo vizuri tunaweza kusimamia mambo yetu wenyewe hili ni jambo jema tumejifunza mambo mengi katika mabanda tuliyotembelea,”amesema
Aidha, amesema anampongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwepo na mazingira mazuri na serikali yake katika suala nzima la amani kwani isingekuwepo maonyesho hayo yasingefanyika.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa