November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wazanzibar waipongeza TanescoTecknolojia ya Uhalisia Pepe

Hamisi Miraji, Timesmajira Online

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutoka visiwani Zanzibar wamelipongeza Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kwa kubuni Teknolojia ya kisasa inayomuwezesha mtu kuona miradi yao bila ya kwenda sehemu husika.

Wazanzibar hao walitua katika jiji la Dar es Salaam wiki iliyopita wakiwa wageni wa CCM Kata 14 Temeke kupitia Jumuiya ya wazazi kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika suala zima la kichama.

Mara baada ya kutua Dar, walitembelea vivutio mbalimbali hapa jijini ikiwemo daraja la Tanzanite, daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni pamoja na Barabara za juu zilizopo maeneo mbalimbali jijini.

Hata hivyo, walipata fulsa ya kutembelea maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama ‘Sabasaba’ na kujionea vitu mbalimbali katika maonesho hayo.

Walipokuwa katika maonesho hayo, wametembelea banda la Tanesco na kujionea Teknolojia ya kisasa iitwayo Uhalisia Pepe (Virtul Reality), inayomuwezesha mtu kuona mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Julious Nyerere (JNHPP), liliopo kwenye mto Rufiji mkoani Pwani, bila ya kufika eneo la mradi.

Akizungumza mara baada ya kufika kwenye banda la Tanesco kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mfenesini, Zanzibar Kessi Mashaka Ngusa amesema amefarijika sana katika ziara yake hasa alipofika kwenye banda hilo.

“Nalipongeza sana Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kubuni Teknolojia ya kisasa ya uhalisia Pepe yaani (Virtul Reality), ni kifaa kinachonesha ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere liliopo kwenye mto Rufiji.

“Nampongeza marehemu John Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuusimamia vyema mradi huu mkubwa hapa nchini, naamini ukimalizika tatizo la umeme litapungua kwa kiwango kikubwa.

“Amewataka Watanzania kumuamini Rais kwa kile anachokifanya, kuliamini Shirika la Umeme lakini pia kuulinda kwa hali na mali mradi huu kwani una manufaa makubwa sana nchini,” amesema Ngusa.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata 14 Temeke, kupitia Jumuiya ya Wazazi Gogo Mzome ambaye ndiye aliyekuwa mwenyeji wa Wazanzibar amesema kutokana na alichokiona kwenye Banda la Tanesco Sabasaba ni Tecknolijia ya hali ya juu.

“Yaani sikuamini kama nipo Sabasaba jinsi nilivyovaa kifaa cha uhalisia pepe na kujikuta nipo kwenye mradi wa Bwala la Julius Nyerere Rufiji Pwani, Tanesco wanastahili pongezi ya hali ya juu kwa kuwafahamisha wananchi kuhusu mradi huo bila ya kufika eneo husika,” amesema Gogo Mzome.

Ameyataka Mashirika mengine kuiga mfano wa Tanesco, kwani wamepiga hatua sana kuhakikisha wananchi wanajua miradi mbalimbali ambayo shirika hilo linasimamia, hususani inayohusu Umeme.