November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Pinda atoa agizo usimamizi vikundi vya mkopo ya Wanawake

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, amemwagiza Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jerry Silaa, asimamie vikundi vya Wanawake wa Ukonga Ili waweze kupata mikopo .

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, alisema hayo wakati wa kufunga semina ya Wanawake wa Pugu iliyoandaliwà na Diwani wa Pugu Imelda Samjela.

“Nawaomba Wanawake wa Pugu muunde vikundi kwa ajili ya mikopo vikundi watu ambao mnafamiana namwagiza Mbunge wenu atavisimamia Ili muwezeshwe mikopo”alisema Pinda .

Pinda alisema baadae watakutana na vikundi vyote Ili kufanya tathimini na kuvitambua rasmi Ili kuvisimamia.

Alisema katika vikundi changamoto maneno hayakosi badala yake amewataka wasimame imara waweze kuaonga mbele .

Katika hatua nyingine Pinda alisema ifike wakati sasa tufamiane chimbuko la chama cha Mapinduzi kipo chini kwa Wajumbe wa mashina hivyo chama kishuke kwa Wajumbe wa mashina kuwa nao karibu kila tawi waunganishe mashina .

Aidha alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania ,Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa katika sekta na kisiasa hivyo amewataka Watanzania kuunga mkono Juhudi za Rais katika kuleta Maendeleo na kusimamia Miradi ya Serikali .

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa chama Cha Mapinduzi CCM Taifa (MNEC)Simba Juma Gadaf aliwataka Madiwani na Wabunge kuwasimamia wakuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Ili Wanawake wa vikundi waweze kupata mikopo ya Serikali .

Akizungumzia Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa Dar es Salaam alisema CCM itaendelea kushinda chaguzi zake zote na Dar es salaam itakuwa ngome ya chama Cha Mapinduzi amewataka wana CCM kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo na kutangaza miradi ya maendeleo na kuisimamia ambayo inatekelezwa na Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan ikiwemo miradi ya sekta ya afya ,Sekta ya Elimu na miundombinu ya barabara.

Diwani wa Kata ya Pugu Imelda Samjela alisema Wanawake wa Pugu wamepata Mafunzo ya siku tatu awamu ya kwanza semina ya awamu ya tatu kabambe inakuja hivi karibuni wanawake wote wa Pugu watajifunza semina hiyo Ili wajikwamue kiuchumi .

Diwani Imelda aliwapongeza Wanawake wa Pugu wa mafunzo hayo wote wameelewa watumie vizuri Elimu hiyo katika shughuli zao za ujasiriamali na kuwataka wajiunge Brela mwakani watapata fursa ya kushiriki maonyesho ya Biashara Sabasaba .

Katika semina hiyo wageni mbalimbali waalikwa walikuwepo akiwemo Mwenyekiti wa CCM mkoa Dar es Salaam ,Abas Mtemvu ,Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Ojambi Masaburi ,Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa na Madiwani wa Viti Maalum Moza Mwano na Mwl,Beatrice Edward.