Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
MAMLAKA ya Elimu ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) imesema vijana wa kitanzania itumie fursa ya mafunzo ya ufundi stadi kutokana na kuwepo kwa ajira katika mapinduzi ya viwanda nchini.
Hayo ameseyasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la VETA kwenye maonesho 47 ya Biashara Kimataifa Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Kasore amesema kuwa serikali imewekeza nguvu katika ujenzi wa vyuo mafunzo ya ufundi stadi katika kuhakikisha vijana wanapata ujuzi wa kuweza kuajiriwa na kujiajiri pasipo kuwepo kwa changamoto.
Amesema VETA inatarajia kujenga vyuo 64 ikiwemo kimoja cha Mkoa wa Songwe na vingine vyote vya wilaya.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â