Na Mwaisaka Israel, TimesMajira Online
Wakazi wa kata ya Mambwe kenya wilaya ya kalambo mkoani Rukwa wanalazimika kuchangishana fedha kusafirisha wagonjwa hususani Wajawazitto kuwapeleka katika kituo cha afya cha mwimbi kilichopo umbali wa zaidi ya kilometa 30 kwenda kupata matibabu.
Wakizungumza mbele ya mkuu wa wilaya Razaro komba wamesema kuwa kata yao yenye vijiji vitano inahudumiwa na zahanati iliyopo katika kijiji cha madibira na inapotakiwa kupata matibabu ya juu ulazimika kufuata huduma hiyo mbali ambapo wengi wao hawana uwezo wa kiuchumi hivyo uamua kuchangishana ili kuweza kuokoa uhai wa Wananchi wao.
Wamesema kuwa kata hiyo ya MambweKenya ina idadi kubwa ya watu na kuwa wapo mpakani kabisa mwa nchi ya Zambia hivyo wameomba wajengewe kituo cha afya ili waweze kuondokana na adha hiyo na kuwa na uhakika wa afya zao.
Mashaka Sichilima alidai kuwa uchumi wao ni duni sana kwa maana wanategemea sana kilimo hivyo uwezo wa wao kuendelea kuchangishana kuwasafirisha wagonjwa hawana hivyo ni wakati sasa kwa serikali kuwapelekea kituo cha afya ukiolinganisha na idadi kubwa ya watu waliopo katika eneo hilo.
Sambamba na hilo pia wananchi hao wamemweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa wana changamoto nyingine kama ya mawasiliano ya simu hawana mawasiliano kabisa na kuomba wapelekewe minara ya simu ili na wao waendelee kupata huduma ya mawasiliano.
Wamedai kuwa kata hiyo ipo mpakani mwa Tanzania na Zambia na kukosekana kwa mawasiliano ni tatizo kubwa kwao na kuomba mchakato wa jambo hilo ungeanza mapema.
Lakini pia eneo hilo bado lina tatizo kubwa la maji licha ya kuwepo kwa mradi wa maji eneo hilo lakini maji bado hayajasambazwa kwa wananchi na kujikuta wanatumia muda mwingi kutafuta maji na ambayo pia usalama wake ni mdogo sana kiafya.
Kufuatia hari hiyo mkuu wa wilaya Razaro komba alimtaka mkurugenzi mtendaji kuanza mchakato wa kuwa na kituo cha afya katika kata ya Mambwe Kenya na kuwa katika mipango yao ya halmashaur sasa waweke mipango ya kujenga kituo cha afya.
Alidai kuwa kata hiyo ni kubwa na ina vijiji vitano na si vyote vina zahanati hivyo ni muhimu wakaipa kipaumbele kata hiyo katika kuwapatia kituo cha afya sambamba na huduma nyingine walizoziomba na kuwa ni muhimu sana kwa sababu kwanza wapo mpakani kabisa mwa nchi kiasi cha kuhitaji huduma za jamii kwa wingi.
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Nicholaus Mrango alisema kuwa wameagiza wananchi kuanza kujenga kwa kutumia nguvu zao na wao watawapelekea wataalamu na kama wakifika kiwango cha renta halmashauri itawaongezea nguvu ili mwisho siku waweze kupata kituo cha afya na kimsingi wanatakiwa kuwa na kituo cha afya.
Kuhusu huduma nyingine kama za mitandao ya simu serikali ilishaanza kulifanyia kazi kwa maana mamlaka ya mawasiliano TCRA walipelekwa eneo hilo na kujionea uhitaji wa eneo hilo kuwa na minara ya mawasiliano na kwamba serikali inalishughulikia.
Kuhusu suala la maji amesema kuwa serikali imepeleka mradi mkubwa wa maji na sasa wanaendelea kuhakikisha kuwa maji yanasambazwa kwa wananchi na kuwa hilo litakamilika ndani ya muda mfupi.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba