Na Hadija Bagasha, Timesmajira Online TANGA
TAKWIMU zinaonyesha kwamba idadi ya waraibu wa dawa za kulevya wanapata huduma ya Methadone katika Kituo cha MAT kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga imekuwa ikiongezaka kutoka watu 173 mwaka 2020 hadi kufikia 896 mwezi May Mwaka 2023.
Hayo yalibainishwa na Kaimu Mkuu wa Kituo cha Methadone (MAT) Dkt Joyce Diwi wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu ya huduma ya Methadone na kupinga matumizi ya dawa za Kulevya Mkoa Tanga Yaliyofanyika kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.
Alisema kwamba usajili huo wa wagonjwa wanaopata huduma (MAT) kutoka Asasi za Kiraia Tatu ambazo ni Gift Of Hope,Tanga Drug Free na Organization Risk Behaviors ambao wamekuwa mstari wa mbele kudhibiti dawa hizo kwenye jamii.
Dkt Joyce alisema kwamba takwimu zinaonyesha kwamba mwezi June 2020 hadi Desemba 2020 walisajili waraibu 173 na wanaume 162 na wanawake 11 huku Januari 2021 hadi Desemba 2021 walisajili waraibu 317 na kuwa na juma la waraibu 490 ambao kati yao kuwa wanawaume 476 na wanawake 12.
Alisema kwa upande wa mwaka 2022 walisajili kuanza mwezi Januari hadi Desemba 2022 waraibu 296 na kufanya jumla ya waraibu 786 wanaume 767 na wanawake 19 huku mwezi January hadi May 2023 wakisajili waraibu 107 na kufanya jumla ya waraibu 896 ambapo kati yao wanawaume ni 876 na wanawake 20.
Aidha alisema hivyo ni Dhahiri inaonyesha kwamba kwamba huduma za MAT ni muhimu kwa jamii kwani ni njia mojawapo ya kupunguza vitendo vya kihalifu katika jamii na kuongeza nguvu kazi ya Taifa na kupunguza kasi ya magonjwa ya kuambukizi na yasiambukiza kama vile moyo,akili kwa kuepuka matumizi ya dawa za kulevya kupitia Mat.
Aliongeza pia ni maendeleo mazuri kwa wagonjwa waliofanikiwa kufuata taratibu za tiba ikiwemo maelekezo ya wataalamu kuhakikisha afya zao zinakuwa bora ingawa
Awali akizungumza wakati wa madhimisho hayo Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Japhet Simeo alisema kwamba wanamshukuru Rais Samia Suluhu kwa kutoa fedha kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwenye Hospitali hiyo.
Dkt Simeo alisema wanamshukuru kutokana na uwepo wa kituo hicho katika Hospitali hiyo ambacho kimekuwa msaada mkubwa kwa waraibu na hivyo kusaidia kuwabadili baada ya kumaliza muda wao.
Aidha pia alisema kwamba wazo la waraibu kujengewa uwezo ikiwemo ufundi,ujasiriamali,bustani kutokana na kwamba vijana wanaotumia dawa ni wapo wengine ni wataalamu wana ujuzi na wengine hawana .
Aliongeza kwamba ni muhimu kujengewa uwezo ili waweze kupata ujuzi ambao utawasaidia kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo hatua ambayo itawaepusha kurudi kwenye matumizi hayo baada ya kumaliza.
“Tutengeneze eneo la ufundi ambalo watakuwa wanatengeneza vitu kwa ajili ya kuuza hivyo siku wakimaliza waweze kupata mitaji ya kujiendeleza hilo wazo hilo nalichukua na nitakwenda kulifanyia kazi”Alisema
,kwenye matibabu ya uraibu zipo adhabu ndogo ndogo maana watu ,suala la mikopo,wakilifanyia kazi wazo lao,
Baadhi ya waathirika wa dawa za kulevya Mkoani Tanga wameishukuru serikali kwa kuwafikishia huduma ya dawa za Methadone katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tanga ya Bombo inayoendelea kuwatibu waathirika wengi wa dawa za kulevya Mkoani Tanga ikiwa ni pamoja na tiba za kisaikolojia zilizokwenda kuwabadilisha mienendo yao na hatimaye kuleta mabadiliko ya kitabia.
Katibu mtendaji wa asasi ya Gift of hope foundation Said Bandawe alitoa shukrani za dhati kwa serikali chini ya uwezeshaji wa mamlaka ya udhibiti wa kupambana na dawa za kulevya (DCEA) kwa kuwezesha huduma bora kwa waraibu wa dawa za kulevya Mkoani Tanga.
Zaidi ya waathirika wa dawa za kulevya 300 wamejitokeza katika Maadhimisho hayo yameandaliwa na taasisi ya Gift of hope foundation kwa kushirikiana na ofisi ya Mganga mkuu wa Mkoa pamoja na wadau mbalimbali lengo likiwa nikupinga na kupambana na matumizi ya dawa za kulevya ambapo maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo Zingatia utu boresha huduma za kinga na tiba.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa