January 1, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TAWA yapokea watalii 120

Na Mwandishi wetu, timesmajira

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini,(TAWA) imepokea jumla ya watalii 120 waliotembelea na kutalii katika Hifadhi ya Magofu ya kale Kilwa Kisiwani na Songo mnara kuridhishwa na utalii wa kutumia boti la kisasa lenye kioo maalum.

Taarifa iliyotolewa  na Ofisa habari wa Mamlaka hiyo Beatus Maganja amesema watalii hao walifika katikahifadhi hiyo Juni 17 mwaka huu na kutembea katika hifadhi hiyo.

Amesema hifadhi hiyo  imendelea kuwa na mvuto mkubwa kwa watalii wa ndani na nje kutokana na mapinduzi makubwa ya kimiundombinu yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi imara wa Dkt. Samia Suluhu Hassan .

AlisemaTAWA imeendelea kuhamasisha watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani kutembelea hifahi hiyo kujionea mapinduzi ya Utalii yaliyofanywa na serikali.

‘’Utalii wa boti la kioo linamuwezesha mtalii kuona viumbe hai vilivyopo chini ya bahari ambapo boti hii  ilizinduliwa mapema mwaka huu na Waziri wa Maliasiri na Utalii Mohammed Mchengerwa,’’amesema.

Kwa Upande wa Watalii hao waliotembelea hifadhi hiyo wamesema matarajio yao yamefikiwa kwa kiwango cha juu zaidi ya walivyofikilia awali kabla ya kufika katika hifadhi hiyo kutalii na kuliona boti hilo la kisasa.