Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa amewataka wakulima wa Skimu ya Mahenge Wilayani Korogwe kulinda vifaa vya ujenzi vitakavyotumika wakati wa Ujenzi na ukarabati wa Skimu hiyo ili kupata mradi wenye ubora na viwango stahiki.
Akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi eneo la mradi mkandarasi Gilco Construction Company ltd, Bw. Mndolwa amefafanua juu ya madhara yanayoweza kujitokeza na kuathiri mradi endapo hatua za pamoja za kidhibiti ulinzi wa malighafi hazitazingatiwa.
” Mkiiba simenti mkandarasi hatanunua simenti nyingine badala yake atapunguza kiwango Cha simenti wakati wa Ujenzi na matokeo yake mradi hautakuwa na ubora wa kiwango kilichokisudiwa na mvua ya masika ikija itausomba mradi wote.”
Aidha Mndolwa amewaasa wanaanchi wa Korogwe kuwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeanza zoezi la Usanifu katika Bonde la mkomazi Kwa gharama ya Tsh. Bilioni 22, Kwa Lengo la kujenga Bwawa na skimu za Umwagiliaji na kwamba zoezi la ujenzi wa Skimu litakapomalizika wenye mashamba makubwa watapunguziwa ili wananchi wengine wasio na mashamba wapewe.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Korogwe mjini, Jokate Mwegelo amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuchangamkia fursa ya Kilimo cha Umwagiliaji ili kuinua maisha na pato la mtu mmojammoja na taifa kwa ujumla, huku akiwasisitiza waache tabia ya kuuza ama kukodisha mashamba yao.
Hata hivyo mkurugenzi wa halmashauri ya Korogwe mji Bw. Tito Mganwa amewaagiza wataalam wa Ofisi yake kushirikiana Kwa karibu na wataalam wa Tume wakati wa ujenzi na ukarabati wa Skimu hiyo ili kupata matokeo chanya Kwa manufaa ya wananchi wa Korogwe na Mkoa wa Tanga Kwa ujumla.
Baadhi ya wakulima wa skimu ya Mahenge wameishukuru serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji NIRC kwa kutenga zaidi bilioni 1.85 kwa ajili ya ukarabati miundombinu ya umwagiliaji katika skimu hiyo.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â