Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline, Chamwino.
KATIBU Mkuu wa CCM Daniel Chongolo ameaigiza Wizara ya Kilimo kukutana na kukaa na Wizara ya Fedha kujadili namna ya kuendeleza miradi ya kilimo ili imalizike ndani ya muda mfupi kwani imeonekana kikwazo ni pesa kutowafikia wakandarasi kwa wakati.
Chongolo ametoa agizo hilo Wilayani hapa jana alipotembelea mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Jenga Kesho Bora uliopo Chinangali Wilaya ya Chamwino na Mashamba ya ushirika wazabibu .
Amesema dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona miradi ya kilimo inaleta tija kwa haraka,hivyo haileti maana kuona kuna miradi yenye majina mazuri lakini haina tija kwa wananchi.
“Dhamira ya Rais kwenye hii miradi ni kuona tija inapatikana haraka,tumeona yule mkandarasi tuliyemkuta kule mkombozi Iringa tumeona wameweka nguvu kuona wanamaliza kwa haraka ,tuwaona Wizara mnavyoendelea kukimbizana lakini nao hapa kuna kakikwazo sisi kazi yetu ni kutatua na kukwamua mahali panapo kwama,Nimezungumza na Waziri wa fedha asubuhi kumuuliza shida iko wapi kaniambia usiwe na wasiwasi mkuu nitakaa nao tutaliweka sawa,
“Sasa nendeni mkakae mje mtupe majibu angalau ndani ya muda mfupi ni namna gani mnaenda kuendelea spidi ya utekelezaji wa miradi hii ambayo inadhamira yakuja na uhakika wa kilimo cha umwagiliaji kwa mwananchi ili malengo ya Rais na Serikali yafikiwe kwa muda uliokusudiwa kama yalivyokusudiwa kwa wananchi hakutakuwa na maana kuwa na miradi yenye majina mazuri na yenye dhamira njema halafu isilete matokeo kwa wakati kwahiyo lazima hilo mkakae kwa haraka waziri nimemwambia wa fedha kama kuna changamoto,”amesema
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi