Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Wafanyakazi wa Tume ya Madini wametakiwa kushirikiana kufanya kazi kwa bidii ili kufikia lengo la makusanyo lililopangwa na Serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 la shilingi bilioni 822.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema hayo leo Machi 31, 2023 wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Watumishi wa Tume ya Madini makao Makuu kilichofanyika katika Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Cha Madini (MRI), Jijini Dodoma.
Profesa Kikula amewaasa Watumishi wa Tume ya Madini kuwa na umoja na kutobweteka katika kazi ili kuendelea kuleta matokeo chanya kwenye Sekta ya Madini na kuzidi kufikia malengo ya kukusanya maduhuli yanayowekwa na Serikali.
“Bila ushirikiano kwa wafanyakazi hatuwezi kufika popote, nashukuru uadilifu wenu unaonesha wazi kuwa tulipopangiwa kukusanya maduhuli katika mwaka wa fedha 2021-2022 tulifikia asilimia 96,” amesema Profesa kikula.
Kwa upande wake Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma amesema kuwa kutokana na uwepo wa madini ya kila aina nchini, ni vyema watumishi wakapanga mikakati mizuri ya kuhakikisha madini yanalinufaisha Taifa.
Naye Kamishna wa Tume ya Madini, Janet Lekashingo amewataka watumishi kutumia kikao kujadili namna ya kutatua changamoto zilizopo katika Sekta ya Madini ili mchango wake uendelee kukua kwenye Pato la Taifa.
Wakati huohuo Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, ubunifu, nidhamu pamoja na kupendana.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa