Na Patrick Mabula, TimesMajira Online Kahama
Serikali imeombwa kutoa elimu ya kilimo kwa vijana ili waweze kuondokana na dhana potofu ya kuona kuwa kulima ni kama adhabu.
Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Mzalendo Foudition na mkulima wa kata ya Kilago , wilaya ya Kahama , Khamis Mgeja,wakati akiongea na wakulima na maofisa ugani katika kijiji cha Lowa Kata ya Kilago,Manispaa ya Kahama.
Ambapo amesema kuwa kilimo kina fursa nyingi za kuweza kujiajiri huko vijijini badala ya kuwaacha wakakimbilia mijini inapaswa vijana wapewe elimu na wawezeshwe ili wajiajiri katika sekta hiyo ambayo itawasaidia kujikwamua kimapato na kuchangia pato la taifa.
Mkuu wa Idara ya kilimo wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Jeremiah Inegeja amesema kuwa sekta ya kilimo ina ajira nyingi mbalimbali zikiwemo za ufugaji na kuomba uwepo ushirikishwaji katika suala la kutoa elimu ili watu wasikichukie kilimo kutokana na mapokeo mabaya yaliyopitwa na wakati.
Mjumbe wa kamati ya mradi wa PETS , unaofadhiliwa na The Foundition for Civil Society wa Kata ya Igunda na kutekelezwa na Chama cha Wasioona Mkoa wa Shinyanga Charles Kafuku ameiomba serikali kuongeza kuajiri maofisa ugani weweze kuwasaidia watu katika suala la kuwapatia elimu ya kilimo chenye tija huko vijijini .
Kwa upande wake muwezeshaji katika mradi PETS katika mfumo wa ufatiliaji wa matumizi ya raslimali za umma katika sekta ya kilimo , Dickson Maganga amesema bado kuna changamoto nyingi katika suala la kilimo ikiwemo uelewa mdogo wa wakulima katika matumizi ya mbolea na upatikanaji wa pembejeo kwa wakati.
Mkulima wa kata ya Kinamapula , Emmanuel Andrew ameiomba serikali iwekeze elimu na teknolojia ya kilimo katika vichwa vya vijana ili iweze kuwasaidia kujiajiri na kwa upande wa pembejeo za kilimo ziweze kupatikana vijijini kwa wakati na Tanzania bila njaa inawezekana.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria