October 1, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Siku ya Uhandisi Duniani kuadhimishwa Dar

Na Jackline Martin, TimesMajira online

Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET) ikishirikiana na Chama cha Wahandisi Washauri Tanzania (ACET) na Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB) zinaungana na Taasisi zote za kihandisi Duniani kupitia shirikisho la Taasisi la Kihandisi la Afrika Mashariki (EAFEO) na shirikisho la Taasisi za kihandisi la Afrika (FAEO) kuadhimisha siku ya uhandisi Duniani itakayofanyika Machi 4, 2023

Tarehe 25 Novemba 2019 kutokana na pendekezo la shirikisho la Taasisi za kihandisi Duniani , shirika la umoja wa kimataifa (UNESCO) lilipitisha na kutangaza tarehe 4 Machi ya kila mwaka kuwa siku ya uhandisi Duniani ambapo wadau wote wa Sekta ya Uhandisi Duniani wanaadhimisha siku hiyo.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam amesema maadhimisho hayo yatahudhuriwa na washiriki zaidi ya 200 kutoka Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi, yatakayofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam

Amesema lengo la maadhimisho hiyo ni kutoa fursa ya kutambua na kuthamini mchango wa uhandisi na watekelezaji wa kazi za kiuhandisi kuleta maendeleo endelevu kwa Taifa.

Pia amesema Lengo lingine ni kuboresha uelewa wa Umma kuhusu jinsi uhandisi na teknolojia vilivyo na umuhimu kwa maisha yetu ya kila siku katika ulimwengu wa sasa.

“Ni fursa ya muhamasisha na muhimiza vijana (wakike na kiume) ambao ndiyo Taifa la kesho kuingia kwenye uhandisi ili kuhakikisha utekelezaji endelevu wa malengo ya maendeleo endelevu kwa miaka mingi ya mbele na Vizazi vijavyo.”

Aidha alisema kama jamii ya wahandisi wanapaswa kuwa na jitihada za pamoja ili kuokoa ufaulu wa wanafunzi katika masomo ya sayansi kwani kwa miaka ya hivi karibuni ufaulu wao umekua ukishuka.

Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni ‘Ubunifu wa Uhandisi kwa ulimwengu unaostahimili zaidi’ ambayo inazingatia kuwa Dunia ipo kwenye zama za utandawazi ya Karne ya 21 ambayo Maendeleo yake ni makubwa na yanachochewa zaidi na mapinduzi ya kidigitali.