Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Diwani wa Kata ya Kipawa Kwezi awasilisha ILANI ya chama cha Mapinduzi CCM na kuelezea mafanikio ya Kipawa sekta ya Elimu Halmashauri ,wahisani na Wananchi kwa ujumla wamepokea kiasi Cha shilingi 837,457,800 katika kutekekeza miradi mbalimbali katika sekta ya Elimu kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya Madarasa .
Diwani Aidan Kwezi alisema pia kiasi cha shilingi 112,521,365 zimetumika kugharamia Shughuli za utawala katika shule za msingi katika kipindi cha 2020 2022 .
Diwani Aidani alisema pia wamepokea Jumla ya shilingi 52,427,125 kwa ajili ya Elimu Maalum shule ya Msingi Air wing.
Aidha Diwani Aidan Kwezi alisema mafanikio mengine Kata ya KIPAWA sekta ya Elimu Msingi shule ya Msingi Majani ya Chai imekuwa English Medium kwa Sasa inafundisha katika mtaala wa Lugha ya Kingereza kuanzia January 2023
Alisema Idara ya Elimu sekondari zimeingia shilingi 529,402 ,200 lwa ajili ya Ujenzi wa madarasa pia shilingi 343,340,665 zimetumika katika ujenzi wa mdarasa ya sekondari kuanzia 2022 mpaka 2023.
Alisema shule ya sekondari Ilala shilingi Milioni 80,000,000 zimetumika katika ujenzi wa madarasa manne fedha za pochi la mama shule ya sekondari Minazi mirefu shilingi 160,000,000 zimetumika kujenga vyumba nane vya madarasa chanzo Cha pesa za Mkurugenzi .
Mwenyekiti wa Chama Cha MÃ pinduzi CCM WIlaya ya Ilala Saidi Sidde alisema kata ya Kipawa ni kata kubwa na Viongozi wa Kipawa wote wana uwezo ambapo aliwataka wote kukitetea chama cha MÃ pinduzi CCM Ili kiweze kuendelea kushika Dola .
Mwenyekiti Said Sidde alisema kata ya Kipawa ni kata ya kisasa ina Miradi mikubwa ya maendeleo ambayo imetekelezwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Kuhusu kero za Kipawa Bonde la Mto Msimbazi na SOKO la Kipawa Serikali itatatua hivi karibuni kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli .
Aliwataka viongozi wa Chama kufanya kazi za Chama ndani ya Chama na nje ya Chama katika Utekelezaji wa Ilani .
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kipawa Saidi Mkuwa amewataka viongozi wa Chama Kipawa KUJENGA umoja na mshikamano wawe wamoja kusaka Dola na kufanya kazi za Chama na Serikali .
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba