Na Mwandishi Wetu, Timesmajira, online
Mamlaka ya hali ya hali ya hewa nchini TMA, imetangaza kuwa msimu wa mvua za masika kwa baadhi ya mikoa mingi zinatarajiwa kunyesha za wastani hadi chini ya wastani huku mikoa michache ikipata mvua za wastani hadi juu ya wastani.
Akizungumza wakati wa mkutano na vyombo vya habari leo katika Ofisi za TMA-Dar es Salaam, Ubungo Plaza, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang’a amesema maeneo yatakayopata mvua za juu ya wastani ni pamoja na Dar es salaam mkoa wa Pwani,Unguja na Morogoro kaskazini huku mikoa inayopata mvua A wastani hadi chini ya wastani ni pamoja na na Kagera,Geita,Mwanza ,Shinyanga,Simiyu,Mara,Arusha,Manyara,Kilimanjaro,Tanga pamoja Kisiwa cha Pemba.
Aidha, ameongezea kuwa Ongezeko la mvua linatarajiwa katika kipindi cha mwezi Mei 2023, hususan katika maeneo ya pwani ya kaskazini
Mchambuzi wa Hali ya Hewa kutoka TMA, Rose Senyangwa amesema mifumo ya hali ya hewa joto la bahari la wastani hadi juu kidogo ya wastani linatarajiwa katika eneo la kati la bahari ya pasifiki, joto la wastani linatarajiwa katika eneo kubwa la kitropiki la bahari ya Hindi huku joto la juu ya wastani likitarajiwa katika eneo la Mashariki mwa Bahari ya Atlantiki hali hiyo itadhoofisha mifumo inayosababisha mvua.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi