Na Heri Shaban, TimesMajira Online, Bagamoyo
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Halima ukash ametoa agizo kwa Taasisi binafsi na za Serikali kupanda Miti ya matunda na miti ya kivuli Wilayani Bagamoyo kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serikali kukabiliana na mabadiriko ya tabia ya nchi .
Mkuu wa Wilaya Bagamoyo Halima ukash alisema hayo wakati Benki ya Standard Chartered walipokuwa wakipanda miti kwa ajili ya utunzaji Mazingira shule ya Msingi shukuru Kawambwa .
“Ninaagiza taasisi zote zilizopo Wilayani Bagamoyo suala zima la utunzaji Mazingira katika Wilaya yetu ya Bagamoyo kila taasisi Moja kupanda miti isiyopungua 30 na kila kaya kupanda miti Mitano “alisema Halima .
Mkuu wa WIlaya Halima alisema WIlaya yote tukipanda miti tutalinda vyanzo vya Maji na kukabiriana na mabadiriko ya Tabia ya nchi alitumia fursa hiyo kuwapongeza Benki ya Standard Chartered kwa kupanda miti hiyo na kuwaomba wadau wengine kuunga mkono kampeni ya upandaji miti .
Alisema mtoto umleavyo ndiyo akuavyo wanafunzi wa shule ya Kawambwa watakuwa Mabalozi wazuri katika suala la utunzaji wa Mazingira ya shule yao .
Aliagiza Halmashauri ya Bagamoyo kutenga pesa kwa ajili ya kununua miti wawe na Kampeni endelevu ya upandaji miti na kutunza Mazingira .
Alipiga marufuku kukata miti na utoaji vibari ameshauri sasa waanze kutumia nishati ya Gesi
Afisa Elimu msingi Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Wema Kajigile alisema WIlaya hiyo ina shule jumla 66 wameanzisha Kampeni ya uboreshaji MAZINGIRA kwa kupanda miti 3500 shule zote .
Afisa Elimu Kajigile alisema wanatoa Elimu ya utunzaji mazingira kwa wanafunzi watakapokuwa kila mmoja ajue suala zima la utunzaji wa Mazingira kwa ajili ya kupata hewa safi na kulinda vyanzo vya Maji.
Kajigile alisema mikakati ya wilaya hiyo na malengo waliojiwekea shule Zote za msingi Bagamoyo kuwa ya kijani kwani inawezekana .
Akizungumzia sekta ya Elimu kwa sasa wilaya hiyo inafanya Vizuri matokeo ya mwaka 2022 ufaulu asilimia 94
Mbunge wa BAGAMOYO Mwarami Mkenge alisema serikali ya chama Cha Mapinduzi CCM imefanya mambo makubwa katika sekta ya elimu Wilayani Bagamoyo changamoto mbalimbali zitatatuliwa hivi karibuni ,awali Mfuko wa Jimbo ukitoa msaada wa madawati.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba