October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

U.S Embassy,UTPC yatoa mafunzo kwa Wanahabari 15, kuendana na mabadiliko ya Teknolojia

Na Judith Ferdinand,TimesMajira Online, Mwanza

Kukua kwa teknolojia duniani kunaenda na mabadiliko ya matumizi ya zana katika sekta ya uandishi wa habari, ili kuendana na mabadiliko hayo waandishi wa habari nchini hapa wanapaswa kuwa na uelewa juu ya matumizi ya vifaa hivyo vya kidigitali kati utendaji kazi wao.

Huku wakizingatia maadili ya taaaluma hiyo ili kuwa na vyombo huru vya habari ambavyo ndio chachu ya kuwa na demokrasia yenye nguvu.

Zana hizo ambazo zinarahisisha utendaji kazi kwa waandishi wa habari na kupunguza kubeba vifaa vingi kwa wakati mmoja ni rahisi na nafuu zaidi kwa kundi hilo endapo litapata elimu ya matumizi sahihi kwa kuzingatia maadili ya taaluma hiyo.

Kwa kutambua umuhimu wa kundi hilo katika jamii na kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani Ubalozi wa Marekani nchini hapa kwa kushirikiana na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini(UTPC),imewajengea uwezo waandishi wa habari 15,kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza(MPC),juu ya maudhui mbalimbali(multi-content journalism).

Akifungua mafunzo ya maudhui mbalimbali kwa waandishi wa habari(multi-content journalism training),yaliofanyika Februari 15,mwaka huu wilayani Ilemela mkoani Mwanza,Mkuu wa Kitengo cha Habari Ubalozi wa Marekani( U.S.Embassy nchini Tanzania),Michael Pryor, ameeleza kuwa teknolojia na zana za uandishi wa habari zinaendelea kubadilika.

Hivyo ameeleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwasaidia waandishi wa habari kutumia zana mpya ili kuweza kuendelea kutimiza majukumu yao muhimu kulingana na mabadiliko ya teknolojia.

Pryor amewasisituza washiriki wa mafunzo hayo kuutumia vyema elimu waliopata kwenye kazi zao pamoja na kuwafundisha wengine.

“Tunaamini kuwa na demokrasia yenye nguvu,tunahitaji vyombo vya habari huru ambavyo vinazingatia maadili,jinsi ya kuripoti pande zote bila upendeleo,kutumia vyanzo vingi vya habari, kuchunguza, kuthibitisha na kujumuisha takwimu,hizi zote ni kanuni na msingi wa uandishi wa habari,”ameeleza Pryor.

Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Kenneth Simbaya, ameeleza kuwa mafunzo hayo ni kuwatoa waandishi wa habari mahali wa lipo na kwenda kwenye hatua nyingine kwani kujifunza hakuishi.

“Wote tunafahamu kuwa ulimwengu wote unakwenda kwenye digital (kidigitali),kama unaenda huko na sisi kila wakati tunapopata fursa za kujidhatiti,na kupata fursa ya kuongeza maarifa tuitumue vizuri,kujifunza kunahitaji nidhamu,”ameeleza Simbaya.

Ameeleza kuwa mafunzo hayo yataongeza thamani katika vyombo vya habari ambavyo washiriki wanafanya kazi pamoja na kwenye jamii endapo wataitumia elimu waliopata vyema.

Mtaalamu wa mambo ya habari kutoka Ubalozi wa Marekani Japhet Sanga, ameeleza kuwa uandishi wa habari umebadilika na unaelekea kwenye mitandao hivyo waandishi wa habari wanapaswa kuzingatia misingi ya taaaluma hiyo.

“Maadili ni muhimu sana,tufanye ufuatiliaji wa taarifa,hii itatusaidia kuleta heshima kwa vyombo vya habari za mtandaoni kwa jamii,”ameeleza Sanga.

Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Mariam John, ameeleza kuwa mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kuelewa na kufahamu namna ya kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika utendaji kazi wao wa habari kwa urahisi na haraka.

“Tunaushukuru Ubalozi wa Marekani kwa kushirikiana na UTPC kutupa mafunzo haya,ambayo yametujengwa uwezo sisi wanahabari wa kuweza kufanya kazi zetu kwa urahisi na kutumia vifaa vichache,”ameeleza Mariam.

Baadhi ya washiriki mafunzo ya maudhui mbalimbali kwa waandishi wa habari(multi-content journalism training),yaliofanyika Februari 15,mwaka huu wilayani Ilemela mkoani Mwanza na kuaandaliwa na U.S Embassy kwa kushirikiana na UTPC,wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa katika mafunzo hayo.
Mkuu wa kitengo cha habari Ubalozi wa Marekani Michael Pryor, akizungumza wakati akifungua mafunzo ya maudhui mbalimbali kwa waandishi wa habari(multi-content journalism training),yaliofanyika Februari 15,mwaka huu wilayani Ilemela mkoani Mwanza na kuaandaliwa na U.S Embassy kwa kushirikiana na UTPC.
Mtaalamu wa mambo ya habari kutoka Ubalozi wa Marekani Japhet Sanga,akiwasilisha mada katika mafunzo ya maudhui mbalimbali kwa waandishi wa habari(multi-content journalism training),yaliofanyika Februari 15,mwaka huu wilayani Ilemela mkoani Mwanza na kuaandaliwa na U.S Embassy kwa kushirikiana na UTPC.
Mariam John,mmoja washiriki wa mafunzo ya maudhui mbalimbali kwa waandishi wa habari(multi-content journalism training),yaliofanyika Februari 15,mwaka huu wilayani Ilemela mkoani Mwanza na kuaandaliwa na U.S Embassy kwa kushirikiana na UTPC,akichangia mada katika mafunzo hayo.