Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ORECORP Limited Bw. Henk Diederichs.
Mazungumzo baina ya Waziri Dkt Mabula na Mtendaji Mkuu huyo wa ORECORP Limited yamefanyika jijini Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Dkt Allan Kijazi na Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha.
Kampuni ya ORECORP Limited imeingia ubia na kampuni ya Sotta Mining Limited yenye ubia na serikali na kuunda kampuni ya uchimbaji madini ya Nyanzaga Mining Corporation Limited ambapo Sotta Mining Corporation inamiliki asilimia 84 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamiliki asilimia 16.
kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Nyanzaga inatarajia kuchimba dhahabu eneo lenye ukubwa wa 23.36 kilometa za mraba lilipo vijiji vya Sotta na Nyabila kata ya Igalula wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kwa ajili ya shughuli za uchimbaji na ujenzi wa miundombinu mbalimbali inayotumiwa na mgodi huo ambapo ili kampuni hiyo kuanza shughuli zake inatakiwa kutwaa ardhi kwa mujibu wa sheria kwa kuhakikisha wananchi wanalipwa fidia stahiki na kupisha katika eneo hilo.
Kampuni ya uchimbaji dhahabu Nyanzaga ilitoa kandarasi kwa kampuni ya Uthamini ya Ace Consultants LTD ya kutekeleza zoezi la uthamini wa mali za wananchi wanaotakiwa kupisha shughuli za uchimbaji.
More Stories
Dkt.Mathayo:Dkt.Samia,Dkt.Mwinyi wanastahili,ajivunia mafanikio jimboni
Wanafunzi 3000 wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Rais Samia, Mwinyi ‘mitano tena’ Nchimbi aula