October 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nkasi yapitisha mapendekezo ya bajeti 2023/24

Na Israel Mwaisaka, TimesMajira Online, Rukwa

HALMASHAURI ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imepitisha mapendekezo ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2023-24 kiasi cha Tshs,Bilioni 41.07 kutoka katika vyanzo mbalimbali ambapo Bilioni 3.11 ni makusanyo ya ndani.

Akiwasilisha mapendekezo hayo ya bajeti mbele ya baraza la madiwani afisa mipango na uchumi wa wilaya Nkasi Deusdedith Joseph amedai kuwa bajeti hiyo itatokana na vyanzo mbalimbali ambapo Tshs,21.21 mishahara ya watumishi,Bil.12.3 miradi ya maendeleo na Milioni 882.4 matumizi mengineyo.

Pia alidai kuwa katika fedha hizo Tshs,Bilioni 3.5 ni maombi maalumu ya ujenzi wa soko kuu la kisasa mjini Namanyere wakati katika makusanyo ya ndani Bil.2.1 ni matumizi ya kawaida na Mil.991.9 ni kwa ajiri ya miradi ya maendeleo.

Akitoa ufafanuzi zaidi mbele ya baraza hilo afisa mipango huyo alidai kuwa katika pendekezo hilo la bajeti pia wamependekeza kuwa na mradi wa kimkakati ambao ni ujenzi wa hotel ya kisasa pamoja na ukumbi.

Pia taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilayani Nkasi imetambulisha programmu ya TAKUKURU-Rafiki kwa madiwani na wataalamu wa halmashauri ya wilaya Nkasi ili kuongeza ushiriki wa kila mwananchi na wadau katika kutokomeza tatizo la rushwa katika utoaji wa huduma kwa jamii na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Akitambulisha programmu hiyo kwenye kikao cha baraza la madiwani kaimu afisa TAKUKURU wilaya Nkasi Stivini Nkwera amesema kuwa programmu hiyo inaakisi maana ya neno “Rafiki” kwa kubeba dhana ya kuwa karibu na ushirikiana na Wananchi pamoja na wadau.

Alisema kuwa programmu hiyo itakelezwa kwa kuwa na vikao ngazi ya kata ili kutambua kero zilizopo kwenye utaji au upokeaji wa huduma mbalimbali.

Nkwera alisema kuwa programmu ya “TAKUKURU –Rafiki” itachangia kukuza ustawi wa utawala bora kwa kuzuia vitendo vya rushwa visitokee katika utoaji wa hudumma kwa umma au utekelezaji wa miradi ya maendeleo sambamba na kuokoa fedha za umma kwas kujengwa au kutelezwa miradi bora endelevu na inayokidhi thamani ya fedha iliyotumika.

Madiwani wa halmashauri ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa wakitoa hoja mbalimbali kwenye kikao cha kupitisha pendekezo la bajeti la Bil.41.07 katika mwaka wa fedha wa 2023-24