October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Naibu waziri wa maji Mhandisi Mahundi akabidhi Mtambo wa kuchimba visima kwa mkoa wa Mbeya

Na Esther Macha,Timesmajira, Online, Mbeya

WIZARA ya maji imekabidhi mtambo wa kuchimba visima vya maji katika maeneo ya mkoa wa Mbeya yenye uhaba wa maji ili wananchi waweze kuepukana na adha ya maji ambayo imekuwa ikiwakumba hasa Wilaya ya Chunya.

Akikabidhi mtambo huo Naibu waziri wa maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema kuwa wizara ya maji imekuwa na historia kubwa kwenye upatikanaji wa maji .

Amesema kuwa wametimiza ahadi ya kukabidhi mtambo huo wa uchimbaji visima na kuanzia itaanzia wilaya ya Chunya mkoani Mbeya katika mikoa iliyobahatika kupata mtambo huo mojawapo ni mkoa wa Mbeya .

‘’Nimshukuru Mh .Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa msaada mkubwa kwenye wizara ya maji hasa kwenye maeneo ya pembezoni mwa Miji ambako ndiko kuna changamoto ya maji hivyo tunamshukuru sana Rais wetu , mashine hii ya uchimbaji visima itaanza kwa wilaya ya Chunya na maeneo mengine ya mkoa wa Mbeya ‘’amesema Mhandisi Mahundi .

Hata hivyo Mhandisi Mahundi amesema kuwa kwa maeneo yaliyokuwa hayana historia ya kupata maji sasa yanaenda kuchimbiwa visima vya uhakika wa kupata maji.

Akielezea zaidi Mhandisi Mahundi amesema kuwa wanategemea kupata ushirikiano kutoka kwa wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Mbeya kuhakikisha mipango ya uchimbaji visima ambako kuna maeneo kulikuwa na tatizo la maji utekelezaji wa maji unakamilika haraka na ndipo inapatikana kauli ya kumtua ndoo.

‘’Ndugu Mkuu wa mkoa naomba nikukabidhi mtambo huu mkubwa wa uchimbaji visima na sisi kama wizara tutaendelea kufanya kazi na kesho tunapeleka mtambo huu wilaya ya chunya tunaenda kujibu maombi ya wachimbaji wadogo katika eneo la Itumbi wmbao wapo wengi tunarajia wiki ijayo Bi.250 ili mtambo uweze kuanza kufanya kazi kwa ufasaha na tunaenda kuwaeleza wananchi ‘’amesema .

Meneja wa wakala wa maji vijijini (RUWASA) Hans Patrick amesema kuwa mtambo huo utasaidia kuongeza huduma ya upatikanaji wa maji kwa upande wa vijijini kutoka asilimia 63 ya sasa mpaka kufikia asilimia 85 ifikapo 2025.

Amesema kuwa Febuari kulikuwa na utiaji saini mkataba wa maji mto Kiwira ambao utaondoa kero ya maji ambapo waziri wa maji aliagiza kupatikana kwa mtambo wa uchimbaji visima na kuanzia mtambo huo utaanzia uchimbaji visima kwa mkoa wa Mbeya .

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Mbeya , Dkt. Stephen mwakajumulo ameomba kuwe na ratiba ya uchimbaji visima ili kuondoa maneno kuwa mtambo huo unakaa sehemu moja kwa muda mrefu pia kuwepo na utunzaji mzuri wa mtambo huo ili uweze kusaidia maeneo mengine , kwani chunya kwa mkoa wa mbeya ndiko kuna changamoto kubwa ya maji hivyo hichi kifaa tukitunze’’amesema.

‘’Huu mwaka toka tumeanza ni bandika pandua kwetu ni mwaka wa neema kubwa na ni jambo la kujivunia hivyo ni vema miradi tuliyopewa tuitunze kikamlifu ‘’amesema.

Juma Homera ni mkuu wa mkoa wa Mbeya amesema kuwa wanamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa msaada wa mtambo mkubwa wa kuchimba visima ambapo fedha za kununua mtambo huo zimetoka katika maeneo tofauti tofauti .