October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mahundi atembeleaa bwawa la maji taka Kalobe

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi ,Maryprisca Mahundi ametembelea bwawa la Maji taka Kalobe lililopo Jijini Mbeya lengo likiwa ni ni kukagua miundo mbinu ya mtandao huo ikiwa ni mpango wa Wizara ya Maji kuyatumia Maji yanayokusanywa kuyatumia baada ya kusafishwa.

Baada ya kukamilisha ukaguzi Mahundi amepongeza mpango wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya kwa namba inavyotekeleza mradi huo ambapo inaendelea kutoa elimu ili kuongeza mtandao wa watumiaji maji taka kwani licha ya mtandao kufikia asilimia thelathini ni asilimia kumi na tano tu ya wananchi wanaonufaika.

Aidha Mahundi amesema zaidi ya shilingi bilioni nne zimetolewa na Wizara kwa ajili ya kufanya utafiti ili mradi wa Maji taka uwe na tija zaidi ili kulinda mazingira.

“Tunategemea mradi huu utakuwa na matokeo makubwa Sana na manufaa kwa wananchi wetu”amesema.

Kwa upande wake meneja Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya CPA Gilbert Kayange amesema mpaka sasa wamesajili zaidi ya wateja 2900 lakini wanaonufaika ni 2600.Hata hivyo Kayange amesema wanaendelea kutoa elimu ili wananchi wengi wajiunge na mtandao wa maji taka badala ya kutumia vyoo vya shimo sambamba na kuwataka wananchi kuacha kutiririsha hovyo maji.

Kayange amesema endapo wananchi wengi watajiunga na mtandao wa maji taka mabwawa hayo yatazalisha mbolea pia maji yatakayosafishwa yatasambazwa kwa wateja hivyo kuongeza upatikanaji wa maji.

Hata hivyo Kayange amesema pamoja na utekelezaji wa mradi wa maji taka baadhi ya wateja wamekuwa wakitupa taka mwenye mabomba hivyo kusababisha kuziba kwa mabomba.

Endapo elimu itatolewa kwa kushirikiana na Jiji wananchi wengi watajiunga na mtandao hivyo itasaidia kuhifadhi mazingira na kuachana na utumiaji wa vyoo vya shimo.