September 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bodi ya maji,Bonde la Wami Ruvu kuchimba visima kumi kumaliza changamoto ya maji mikoa mitatu

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.

BODI ya Maji ya Bonde la Wami Ruvu imesema kuwa imejipanga kuhakikisha inamaliza changamoto ya tatizo la maji katika mikoa ya Dar es salaam,Pwani na Morogoro kwa kuchimba visima kumi vyenye maji ya kutosha.

Hayo yameelezwa jijini hapa leo,Februari 7,2023 na Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy wakati akizungumza na waandishi wa kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji chini ya bodi hiyo.

Mha.Mmasi amesema kuwa bodi hiyo imejipanga kuhakikisha inatatuza tatizo la maji katika mikoa ambayo imekuwa na changamoto ya maji hususani katika mkoa wa Pwani, Morogoro na Dar es salaam.

“Lengo la kuanzishwa kwa bodi ya maji ni pamoja na kuhakikisha rasilimali za maji zinalindwa,kutunzwa na kuendelezwa  kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho sambamba na kuhakikisha utunzaji wa mazingira,”amesema.

Pia Mmassy amesema kuwa Bodi ya maji imeweza kufanikiwa  kubaini  vyanzo vipya vya maji ambavyo amevitaja kuwa ni eneo la Nzuguni lililopo Jijini Dodoma kuwa linamaji ya kutosha na hivi karibuni litatangazwa katika gazeti la serikali kuwa ni benki ya maji pamoja na Dakawa katika mji wa Dodoma.

Kuhusu utunzaji wa vyanzo vya maji mhandisi Mmasi amesema kuwa wanahakikisha vyanzo vyote vinatunzwa kwa ajili ya kutunza maji yaliyopo chini ya Ardhi huku akiwataka watanzania kuepukana na tabia ya uchimbaji ovyo wa visima vya maji kwa maelezo kuwa kunaweza kusababisha kuchafua maji yaliyopo chini ya ardhi jambo ambalo ni hatari kuweza kuondoa sumu ambayo inaweza kujitokeza.

Amesema mikakati ya Bodi hiyo ni kulifanya Bonde hilo kuwa lenye Mazingira safi na kijani linalotunza na kuendeleza vyanzo vya maji kwa maendeleo ya Binadamu kijamii na kiuchumi yanayostahimili majanga yanayoweza kutona na  maji.

Huku dhima ikiwa ni Kuratibu kwa ufanisi mipango na utekelezaji wa pamoja wa Utunzaji na uendelezaji wa vyanzo vya Maji ili kufikia maendeleo endelevu, jumuishi na stahimilivu ya Bonde.

Hata hivyo amesema ili kukabiliana na changamoto ambazo zinajitokeza katika utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji, Bodi ya Maji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea kutekeleza.

Aidha amesema kuwa Bodi hiyo inatekeleza jitihada mabalimbali ikiwemo tambuzi wa maeneo yatakayo faa kwaajili ya ujenzi wa mabwawa matano likiwemo bwawa la Mandela litakalo tumika katika shughuli za kilimo cha umwagiliaji, Mifugo na shughuli zingine za kijamii,uwezesha shughuli mbadala katika kupunguza kasi ya ukataji miti kwenye vyanzo vya maji kwa kujenga majiko banifu na kutoa miche ya matunda kama vile parachichi.

Kuendelea kuainisha  maeneo ya kipaumbele ili kuyatangaza kuwa maeneo tengefu ya vyanzo vya maji likiwemo eneo la dakawa kwa ajili ya uchimbaji visima vitakavyoongeza uzalishaji wa maji kwa MORUWASA,

Bodi ya Maji kuendelea kufanya tathmini ya kina katika Mito na maeneo yote yanayo sababisha mafuriko na kusababisha maafa (Mito ya Mkondoa, Mkundi, Diwale na Mgeta Chini) na Upandaji wa miti rafiki kwenye vyanzo vya maji.