November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Benki ya NMB yatoa vifaa tiba vya milioni 26 Arusha

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Sekta ya afya ni sekta muhimu kwa maendeleo ya jamii zetu na kwa kulitambua hilio, Benki ya NMB imeshirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya kusaidia kuboresha huduma za Afya kwa Wilaya ya Arusha kwa kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye jumla ya thamani ya zaidi ya sh. 26,000,000 katika kituo vya Afya – Mkonoo ambavyo ni;


✅ Vitanda 10 vya kujifungulia kwa kina mama
✅ Vitanda 10 vya kulazia wagonjwa wa kawaida

Huku, kwa Kituo cha Afya Levolosi waliwakabidhi mabenchi 20 ya kusubiri huduma na kukalia kwa wasindikizaji.

Kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Afisa Mkuu wa Huduma Shirikishi wa NMB, Nenyuata Mejooli alisema kuwa vifaa hivyo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na wao kama benki inayoongoza Tanzania, wanao wajibu wa kuhakikisha jamii inayowazunguka inafaidika kutokana na faida wanayoipata.

Lakini pia, aliongezea kuwa Benki ya NMB imekuwa ikipokea maombi mengi sana ya kuchangia katika miradi ya jamii, lakini benki imejikita zaidi katika maeneo ya elimu, afya, na misaada ya hali na mali katika nyakati ngumu kama za majanga na tumekuwa mstari wa mbele kuchangia huduma za kijamii kwa lengo la kurejesha sehemu ya faida yetu kwa jamii.

kwa zaidi ya miaka kumi mfululizo, Benki ya NMB imekuwa ikitenga asilimia 1â„… ya faida yake kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii inayoizunguka.