Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
MKUU wa mkoa wa Singida Peter Serukamba amezindua zoezi la upandaji miti millioni moja na nusu pamoja na utunzaji mazingira katika wilaya ya Ikungi
Rc Serukamba akiwa ameambatana na secretariat ya mkoa ikiongozwa na katibu tawala wa mkoa wa singida Mwalimu Dorothy Mwaluko pamoja na kamati ya usalama mkoa amewataka wananchi kuhakikisha wanapanda miti kama sehemu ya utamaduni wa kutunza mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi
Rc Serukamba pia amezielekeza halmashauri zote mkoa wa singida kutunga sheria ndogo zitakazowabana wale wote wenye nia ovo na mazingira ili kuhakikisha wananchi wote wanashiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira na kuwaagiza wakuu wa wilaya kusimamia mchakato huo
Katika hatua nyingi RC Serukamba amepiga marufuku tabia ya wananchi kuchoma hovyo mikaa hususani katika kata ya isuna na kuagiza hatua kali zichukuliwe kwa wote wanaoshiriki kuchoma mikaa kiholela
Awali akimkaribisha mkuu wa mkoa katika zoezi Hilo lililoanza mpakani mwa ikungi na singida mjini katika kijiji cha utaho mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry Muro amesema katika kutekeleza maagizo ya upandaji miti na utunzaji wa mazingira kuanzia January mpaka sasa tayari zaidi ya miti elfu hamsini na tank imeshapandwa katika maeneo mbalimbali ya umma na binafsi na pembezoni mwa barabara kuu za singida kwenda dodoma na ile ya singida kwenda manyara kupitia babati na zoezi Hilo litakuwa endelevu kwa mwaka mzima na kuwataka viongizi kuanzia ngazi ya vitongoji na vijiji kwenda kata mpaka wilaya kuhakikisha wanajiwekea utaratibu maalum wa kuratibu zoezi hilo kuanzia hatua ya upandaji mpaka ukuzaji wa miti hiyo kwa kushirikishana kwa pamoja
Akitoa salamu za wananchi wa jimbo la singida mashariki na singida magharibu Mbunge wa singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu amewappngeza viongozi wote wa wilaya na halmashauri kwa kuanza utekelezaji wa maazimio ya bunge katika upandaji miti na kutunza mazingira na kusisitiza kuwa wilaya ya ikungi lazima iwe mstari wa mbele katika kuongoza mapambano ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kupanda na kulinda miti kwa nguvu zaidi
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya ikungi Ali Juma Mwanga amesema wamepokea maelekezo ya mkuu wa mkoa yanayowataka kutunga sheria ndogo za usimamizi wa mazingira ambazo safari hii amesema lazima ziwe na makali ya kuhakikisha wananchi wanafuata na kuzingatia kanuni bora za utunzaji wa mazingira ikiwemo miti inayopandwa kwa kasi katika wilaya ya ikungi pamoja na kuhakikisha wanadhibiti tabia za baadhi ya wananchi kuvamia na kukata miti katika maeneo ya Hitachi za misitu ya asili.
More Stories
SACP Katabazi: Elimu ya usafirishaji wa kemikali bado ni muhimu kwa watanzania
REA yajitosa kwenye nishati safi ya kupikia
Maghorofa Kariakoo mikononi mwa Tume