Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
MBUNGE wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu, amegawa majiko ya gesi 150 Bure kwa Mama lishe na Baba Lishe wa soko la Kisutu wilayani Ilala .
Mbunge Zungu aligawa majiko ya Taifa gesi soko la Kisutu Leo kwa Wajasiriamali wa soko hilo mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija .
Akizungumza wakati wa kugawa majiko ya gesi ya Taifa gesi Mbunge Zungu alisema kauli mbiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan, kumtua Mzigo wakuni mama Kichwani katika kata ya Kisutu Jimbo la Ilala nimetekeleza .
“Hivi Karibuni nchi yetu ilikumbwa na janga Wananchi wanateseka na maji ,maji ni uhai bila maji uwezi kuoga wala kupika wala kufanya Shughuli yoyote ya kijamii “alisema Zungu.
Mbunge Zungu alisema gharama ya nishati ya mkaa ni kubwa amewataka mama lishe na Baba Lishe wa kisutu watumie nishati ya gesi Taifa kwa matumizi yao mbalimbali .
Aliwataka viongozi wa chama Kisutu na Serikali ya Mtaa huo kuwa walinzi katika majiko hayo ambayo yametolewa Bure soko lote masharti yake gesi ikimalizika ujaze kampuni ya Taifa Gesi .
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu akiwa jimboni anatekeleza Ilani ya chama kwa vitendo .
Mkuu wa Wilaya Ludigija alitumia nafasi hiyo pia kuwapongeza Kampuni ya Gesi ya Taifa gesi wamekuwa WAZALENDO wanaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanikisha Wananchi watumie nishati ya gesi waachane na kuni na nishati ya mkaa .
Aidha katika hatua nyingine alimpongeza mbunge kutafuta wawekezaji kugawa gesi hizo lengo la Rais wetu zuri, kuwatoa watu Barabarani Wafanyabiashara kuwapeleka maeneo Rasmi Ili waweze kutambulika kwa urahisi limeweza kuzaa matunda Leo wanazawadiwa gesi Bure .
Alisema miti mikubwa iliyokatwa na kusababisha ukame inasababishwa na wakazi wa Dar es Salaam kutumia mkaa hivyo aliwataka Wananchi kutumia Gesi kuacha mkaa inasababisha uhalibifu wa mazingira.
“Taifa gesi ni gesi nzuri inazalishwa nyumbani hivyo Wananchi watumie wamewekeza katika nchi yetu inapatikana nchi nzima alisema Ludigija”
Wakati huo huo Ludigija aliwataka Wafanyabiashara wa mama lishe na Baba Lishe wa Kisutu tukifika mwaka 2024. na Mwaka 2025 wajiandikishe waweze kupiga kura Kumpa ushindi wa kishindo Rais wetu Samia Suluhu Hassan na Mbunge waJimbo la Ilala Mussa Zungu .
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde alipongeza viongozi wa serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Naibu Spika Kwa Kufanya KAZI kwa vitendo.
Mwenyekiti Sidde alisema nishati ya gesi ni Bora inawaepusha na magonjwa ya mapafu,mkaa unachafua Mazingira wasikate miti ovyo.
Meneja wa Mahusiano wa Taifa Gesi Angel Mwita alisema Taifa Gesi ni kampuni inayosambaza gesi ya Taifa Gesi na Mihani leo tumegawa majiko ya gesi 150 kwa ajili ya kujali Afya kwa Wafanyabiashara wa kisutu Jimbo la Ilala kuunga mkono Juhudi za Mbunge Mussa Zungu .
Angel Mwita alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano alieleza watu watumie Gesi ya Taifa Gesi ni safi na Salama ni gesi yetu bohari kubwa ipo hapa nchini .
Alisema wapo Tayari kushirikiana na serikali kuakikisha Wananchi wanapata huduma Bora ambapo pia aliwataka wanunue vifaa Bora vya Taifa Gesi zikiwemo bana za kampuni hiyo.
Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto amempongeza Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu zaidi ya shilingi Milioni 7 zimetumika kugawa Majiko ya gesi Ili kuboresha Biashara zao waweze kuwa Katika Biashara za Kimataifa .
More Stories
Maghorofa Kariakoo mikononi mwa Tume
ITA chatakiwa kutoa mafunzo ya viwango vya juu na kasi ya maendeleo ya Kisayansi
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi