Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Zanzibar
MASHIRIKIANO ya Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) yanatarajiwa kuibua kasi ya kiutendaji katika sekta ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu ili wananchi waweze kudhimudu.
Akizungumza Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi (SMZ) Dkt.Mngereza Mzee Miraji katika kikao cha mashirikiano ya kiutendaji kilichofanyika mwisho wa wiki iliyopita katika ukumbi wa Wizara hiyo Maisara Unguja, alisema kupitia vikao vya mashirikiano baina sekta mbili hizo vitasaidia katika kuibua kasi ya utendaji hasa katika sekta ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu zenye kukidhi mahitaji ya wananchi wenye kipato tofauti.
Alisema kwamba kuna mafanikio yameanza kuonekana kupitia vikao hivyo ikwemo kukamilika rasimu mbili ya makubaliano (MOU) zimekamilika kiutendaji ambapo zitarajiwa kusainiwa katika kikao kijao cha ngazi ya mawaziri wa pande zote mbili wa wizara ya Ardhi ya SMZ na SMT.
Dkt.Mngereza alifafanua kwamba ‘MOU’ zilizokamilika ikiwemo ya Shirika la NyumbaZanzibar (ZHC) na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na ‘MOU’ inahusu Wizara ya Ardhina Maendeleo ya Makaazi Zanzibar na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo yaMakaazi (SMT) ambapo kuna mambo mengi ya ushirikiano wamekubaliana ikiwemongazi ya kitalaamu, kubadilishana uzoefu pamoja na mafunzo kwa watendaji wa taasisi mbili hizo.
Pia alisema wizara ya Ardhi ya SMT imepiga hatua zaidi kiutendaji ambapo wana mfumo unayojulikana kwa jina la Intergreted Land Information System unasaidia kutatua changamoto ya urasimu pamoja na kuboresha huduma hivyo wizara yake kupitia Idara ya Kamisheni ya ardhi imeanza maandalizi ya kuwa na mfumo huyo na wamefika katika hatua nzuri.
Sambamba na hayo Dkt. Mngereza alisema wamekubaliana wawe na mashirikiano yatafiti katika sekta ya ardhi na makaazi ya bei nafuu lakini katika kuanzia hilo watakuwana kamati ya pamoja (Joint committee) ambayo imeshaingizwa katika mazungumzo yayanayoendelea baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na taasisi ya Shelterafrique.
Alifahamisha kwamba taasisi ya Shelterafrique inautaratibu wa kutoa mikopo ya beinafuu kwa nchi wanachama zaidi ya nchi 30 na mwaka huu wanatarajia kutakua namkutano pamoja na maonesho ya teknolojia ya ujenzi wa maakazi ya bei nafuu.
Aidha Dkt.Mngereza alisema wizara yake inakabiliwa na changamoto ya wataalamu waupimaji ardhi ndani ya maji (Hydrographic Survey) hivyo wamekubaliana na KatibuMkuu wa Wizara ya Ardhi SMZ watakuwa na mpango mkakati wa kuwajengea uwezowatendaji wao ambapo kila wizara italazimika kuingiza katika bajeti yake.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi(SMT) Dkt. Allan H. Kijazi alisema watahakikisha wanaweka misingi imara kwawatanzania wote kumiliki nyumba za bei nafuu na kuendeleza matumizi ya ardhi bila ya kuangalia tofauti yoyote.
Alieleza kwamba matarajio ya kikao hicho ni kuwa na mifumo ya pamoja ya uboreshwajiwa utoaji huduma kwa viwango vinavyofanana baina ya Taasisi mbili hizo kwa lengo lakukidhi mahitaji ya Taifa.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC),Mwanaisha AliSaidi kupitia kikao hicho aliwaahidi wananchi wategemee mabadiliko katika sekta ya makaazi nakusemba kwamba shirika lake limejipanga kimkakati katika kuhakikisha linatoa huduma ya nyumba bora na salama kwa bei nafuu.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah KyandoMchechu alisema Shirika hilo kwa sasa limejikita zaidi kwenye miradi ya ujenzi ambapo ndio kipamumbele chake kujenga nyumba katika jiji la Dar es Salaam, Dodoma na maeneo ya miji na nyumba hizo ni za ghoroma na bei nafuu.
Kwa upande wa watendaji waliyoshiriki kikao hicho wamezipongeza Serikali zotembili(SMZ na SMT) kwa kuagiza kuweko na mashirikiano ya kiutendaji katika Taasisi ambazo zinalingana kimajukumu na hazimo katika orodha ya sekta ziliyomo katika Muungano.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa