November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti CCM Wilaya Ilala apokea kero za Barabara mbovu TABATÀ

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde ,amesema anatarajia kufanya ziara ya kutatua KERO za Barabara kata ya TABATÀ na Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,Meya wa HALMASHAURI ya Jiji ,Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo na Mhandisi wa Jiji na Meneja wa TARURA Wilaya ya Ilala kwenda kuangalia Barabara mbovu Kata ya TABATÀ .

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde aliyasema hayo Kata ya Tabata Halmashauri ya Jiji la Dar es asalaam wakati wa semina ya chama cha mapinduzi na Jumuiya zake kwa ajili ya kuwajengea uwezo viongozi wa chama waweze kujua majukumu yao.

“kata ya Tabata kubwa ndio Tabata mama imezaa kata zingine zote zilizopo Jimbo la segerea zimezaliwa na TABATA changamoto ya TABATÀ Barabara kata kubwa Barabara za ndani zimeoza kero hii nimeibeba naifanyia kazi naandaa ziara Watendaji wa Halmashauri Mkuu wa Wilaya Meya ,Meneja wa TARURA ,Kaimu Mkurugenzi waje kujionea na kuchukua hatua mara moja ” alisema Sidde .

Mwenyekiti Sidde aliwataka wakazi wa Tabata kuvuta subira Serikali yetu ni Sikivu atafanya ziara hiyo na Watendaji na Wataalam wa Barabara kwa ajili ya Utatuzi Ili Tabata iwe ya kisasa kama kata zingine zilizopo Jimbo la Segerea mfano Kiwalani na Minazi Mirefu Zina Barabara za kisasa.

Diwani wa Kata ya Tabata Omary Matulanga amewapongeza viongozi wa chama na mashina kwa kupewa Elimu waweze kusimamia majukumu yao katika utekekezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi .

Matulanga akizungumzia changamoto alisema Tabata Kisiwani kero mto Tenge ,na Barabara za ndani za Tabata Kisiwani amna Barabara ya lami .

Matulanga alishauri Serikali ijenge Barabara ya Mwananchi kisiwani kwa kiwango cha lami Ili iweze kupunguza Foleni Barabara ya Tabata Segerea magari mengine yawe yanapita mchepuko yasizunguuke mpaka Tabata .

Aidha Matulanga alisema kero nyingine Tabata Kisiwani wanaitaji shule ya Msingi na kituo cha Afya kutoka na jiografia ya kufika Tabata A mbali na Kata hiyo ni kubwa wananchi wengi wanakosa huduma za Jamii karibu na makazi yao.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Side akizungumza na Wana CCM wa Kata ya TABATÀ katika semina ya chama na JUMUIYA Picha na Heri Shaban.
Diwani wa Kata ya TABATÀ Omary Matulanga akipokea cheti kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde January 12/2023 katika mafunzo ya Chama na Jumuiya zake Kata ya TABATÀ Picha na Heri Shaaban.
Katibu wa CCM kata ya TABATÀ Haruna Alphonce akizungumza katika Semina ya Chama na Jumuiya January 12/2023 Picha na Heri Shaban