Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Simanjiro
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Dkt. Suleiman Serera amewataka Wazazi ama walezi kuhakikisha wanaendelea kuwapeleka wanafunzi kuripoti mashuleni bila visingizio vya sare za shule.
Dkt.Serera aliyasema hayo jana wakati akifanya ziara ya kukagua mahudhurio ya wanafunzi waliopaswa kuripoti mashuleni kuanza kidato cha kwanza, ya Wanafunzi wapya wa Shule za wali, darasa la kwanza na wale wanaoendelea waliokwisharipoti Shuleni.
Shule zilizotembelewa jana Mkuu huyo wa Wilaya ni pamoja na Shule mpya ya Sekondari Kitwai ambapo kati ya Wanafunzi 40 waliopangiwa kuripoti katika shule hiyo Wanafunzi 7 pekee ndio walioripoti katika shule hiyo huku wasichana 4 na wavulana.
” Ukiangalia hapa utaona kuwa bado Wazazi ama walezi na viongozi mbalimbali tunalo jukumu kubwa sana la kuendelea kuielimisha jamii yetu juu ya umuhimu wa kuwapatia elimu watoto wetu, hebu angalia wanafunzi waliotakiwa kuripoti shuleni ni 40 lakini walioripoti ni 7 tu, hivyo 33 wote bado wako majumbani” alisisistiza Dkt.Serera.
Alisema ni vema wanafunzi wakafuatikiwa kwa ukaribu ili wawezenkuanza masomo kwa wakati bila kutoa kisingizio chochote kwani Serikali imeruhusu Wanafunzi kupokelewa Mashuleni hata kwa watakaokosa sareza shule.
” Serikali ya awamu ya sita chini ya Mh.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani imeruhusu wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza kuendelea na masomo huku Wazazi ama walezi wakiendelea kukamilisha kutafuta mahitaji muhimu kama share za shule, ili kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo yao” amesema Dkt.Serera.
Kufuatia hilo amewataka Wazazi ama walezi pamoja na viongozi mbalimbali wa vitongoji, Kijiji na Kata kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaotakiwa kuripoti mashuleni wanaripori haraka iwezekanavyo ili kuweza kuendelea na masomo bila kuingiza suala la kusingizia kukosekana kwa sare za shule.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alisema lengo la ziara yake ni kukagua mahudhurio ya wanafunzi wapya wa Shule za awali, darasa la kwanza, kidato cha kwanza pamoja na wale wanaotakiwa kuripoti kuendelea na masomo, Shule nyingine zilizotembelewa jana na Mkuu huyo ni pamoja Kitwai A, Loondrekes, Lormorijoi na Simanjiro Sekondari.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya aliongozana na Wajumbe wa Kamati ya Usalama Wilaya na Maafisa Elimu wa Msingi na Sekondari ambapo wataendelea kutembelea Shule nyingine kwa wiki hii li kuendelea kujionea uhalisia na kuchukua hatua kwa wale ambao kwa makusudi hawatatekeleza ukumu la kuwapeleka watoto wao mashuleni kama inavyoelekezwa na Sheria na Sera ya Elimu hapa Nchini.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi