Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM WIlaya ya Ilala Al haj Said Sidde, amesema Viongozi wa Chama hicho Pamoja na Jumuiya zake kila mmoja asimamie majukumu yake wasingiliane Majukumu .
Mwenyekiti Said Sidde, aliyasema hayo Jimbo la Ilala katika Semina ya mafunzo ya viongozi wa CCM na Jumuiya zake ya kuwajengea uwezo na kila mtu kumuekeza majukumu yake iliyoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Ilala Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu .
“Natoa agizo kwa Viongozi wa chama na Jumuiya ndani ya Miaka Mitano msimamie utekekezaji wa ILANI na kujenga Jumuiya zenu kila mtu afanye kazi kwa Mipaka yake asimwingilie mwezake” alisema sidde .
Alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Haasan kwa Utekelezaji wa Ilani na miradi miradi ya Maendeleo Alisema Rais ameelekeza shilingi Bilioni sita za skta ya Elimu Wilaya ya Ilala kwa ajili madarasa watoto wetu waweze kusoma .
Aliwataka Wana CCM Wilaya ya Ilala kuunga Mkono utekekezaji Ilani wa Rais Jamhuri ya Muungano Watanzania Samia Suluhu Haasan .
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Wilaya ya Ilala Sidde aliwataka Wana CCM kuonyesha Mshikamano kuwa wa Moja Katika kujenga chama na Jumuiya zake na kutatua kero ngazi ya Kata na mashina .
More Stories
Makalla:Kupanga fujo ni dalili za kushindwa uchaguzi
Tanzania yapanda viwango Utawala wa Sheria Duniani
Rais Samia apeleka neema Tabora