November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhandisi Mahundi kuja kivingine, kuwainua kiuchumi mama lishe wa hali za chini

Na Esther Macha,Timesmajira Online, Mbeya

NAIBU waziri wa maji na Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Mbeya , Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema kuwa wanahitaji kupata wanawake mama lishe wenye hali za chini kiuchumi ili waweze kuwainua kiuchumi na kusonga mbele kimaisha .

Mhandisi Mahundi amesema hayo leo wakati wa kongamano la kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan liloandaliwa na Mbunge wa viti maalum mkoa wa mbeya akishirikiana na umoja wa wanawake Jijini hapa ambalo liliwashirikisha wanawake kutoka wilaya zote za mkoa wa Mbeya pamoja na viongozi wa serikali.

“Mwezi Januari nafasi yangu ya kazi ikiniruhusu nitakuja mawilayani kwenu kitachonileta huko ni wanawake wa mkoa wa Mbeya ambao si wapiga kura si mnazitaka kura za Mama Samia tukiendelea kujifungua ndani hatuwezi kupona lazima tutoke nje tuje tuwape chachu ambao si wana CCM au wapo wapo tu na hawajielewi au wapo kundi lingine nje ya umoja wa wanawake lazima tuwalejeshe ndani ya CCM kupitia umoja wanawake , nataka kila wilaya nije kufanya mashindano ya mama Ntilie wadogo wadogo ,watapika chakula akina mama 70 kwa kila wilaya baada ya hapo tutawaachia majiko ya gesi waweze kupunguza matumizi ya mkaa na kuni”amesema.

Aidha Mhandisi Mahundi amesema kuwa anahitaji mama lishe hali ya chini ambao wadogo wadogo ili tuweze kuwainua na wajue serikali ipo na wajue kuna mwanamke ambaye ni amiri jeshi mkuu lazima wajue kuwa Rais ana wasaidizi wake ambao ni Maryprsica kwa hiyo atafika kila wilaya kwa ajili ya kugawa majiko ya gesi kwa kuwashindisha kwenye upishi .

“Hivi mnafikiri hawa wamama wote 70 kila wilaya tukiwapatia haya majiko naamini hawawezi kumuacha Mama Samia mwaka 2025 lazima kura za mama Samia zitafutwe kwa namna yeyote ile na kitaeleweka tu wanawake tukiamua jambo tunaweza hivyo ndo sababu nasema wanawake wa mkoa wa mbeya tumeweka nadhiri kwa Rais Dkt. Samia Suluhu”amesema .

Mkuu wa mkoa wa Mbeya , Juma homera amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu ni rais mwenye upendo ambaye anajali wanambeya wanawake wanatakiwa kumshukuru Rais kwa jengo la mama mtoto,Rais Samia ameendeleza jengo la mama la mtoto kwa kutoa Bil.7 ili jengo hilo liweze kukamilika .

“Akina Mama leo hii hamuwezi kupata shida tena kwenda mbali kwenda kujifungulia rufaa zote Hospitali ya meta , mkipata nafasi mkatembelee kipo chumba ambacho Mume anasubiri Mke akimaliza ile kazi nyingine ,vituo vya afya vingi Rais Dkt Samia amevijenga kwa wilaya zote “amesema.

Mkazi wa Isanga Jijini mbeya ambaye ni mama lishe EricaMachayo amesema alipatiwa shilingi 50000 akanunua kuku ambao wamwezesha kufika alipo na familia yake kuwa vizuri na kusomesha watoto , wanawake wenzangu tujitume kufanya miradi mbali mbali na hata fedha mnazopewa mkafanyie miradi.

Mariam Habibu mkazi wa Mbarali amesema kuwa mtaji aliopewa na Naibu waziri wa maji umemwezesha kujikwamua kiuchumi kwa kuweza kusomesha watoto wake na kumudu maisha yake.