November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ridhiwani Kikwete atoa agizo Februari Kivule wapate Hati wote

Na HerI Shaaban TimesMajira Online, Ilala

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Ridhiwani Kikwete, amemwagiza Kamishina wa Ardhi Dar es Salaam mwezi February 2023 Wizara yake iwe imemaliza kuwapatia hati za Viwanja wakazi wa Kivule Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam.

Ridhiwani Kikwete, alitoa agizo hilo kata ya Kivule Wilayani Ilala katika mkutano ulioandaliwa na DIWANI wa Kivule Nyasika Getama , wakati wa kukabidhi HATI za viwanja kwa Wananchi wa eneo hilo ambao waliomba toka mwaka 2017 .

“Natoa agizo kuhusiana na maeneo yaliokwama yenye changamoto mpaka kufika February 2023 kazi iwe imeisha Kivule kila Mwananchi awe na hati yake “alisema.

Kikwete Alimwagiza Diwani wa Kivule Nyasika Getama na Watendaji wake kutoa elimu na kuhamasishana Wizara itampa ushirikiano katika changamoto hiyo ya muda mrefu Ili waweze kupewa hatiAlisema Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan, imejipanga kero za Mipango Miji zinatatuliwa na kuwataka Wananchi kulipa kodi ya Ardhi kwa wakati .

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete ameagiza ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dar es Salaam kuitisha mimala ya wananchi wa kata ya kivule wasiopatiwa hati katika zoezi la urasimishaji makazi holela ili waweze kutatuliwa changamoto katika zoezi hilo.

“Kwa kuwa wananchi waliorasimishiwa makazi yao waliacha namba zao za simu basi Kamishna itisha miamala ya wale waliolipa na kuwaelekeza ni kitu gani cha kufanya ili waweze kupata hati’’. alisema Katika mkutano huo.

wananchi wa kata ya Kivule walimueleza Naibu Waziri wa Ardhi kuwa, pamoja na wao kulipa 160,000 lakini wameshindwa kupatiwa hati na kueleza kuwa kumekuwepo mawasiliano hafifu baina ya wananchi na kamati zinazosimamia zoezi hilo.

Wananchi hao wa Kivule pia walishusha lawama kwa Chuo cha Ardhi Morogoro (ARIMO) kuwa kinachelewesha kukamilisha zoezi la urasimishaji katika mitaa ya Kivule.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dar es Salaam Shukran Kyando, Chuo cha Ardhi Morogoro kimefanya kazi kwa zaidi ya asilimia 80 lakini fedha zilizotolewa na wananchi katika zoezi hilo ni asilimia 11 pekee.

“Kata ya Kivuke ina mitaa minne na Chuo cha Ardhi Morogoro kimeingia mkataba wa kufanya kazi katika mitaa hiyo kwa ajili ya kumalizia kazi ya urasimishaji lakini zipo changamoto mbili yaani upande wa kampuni na ule wa wananchi kutolipia viwanja zaidi ya 7000 ambavyo vimeidhinidhwa” alisema Kyando.

.Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Ridhiwani Kikwete akizungumza na Wakazi wa Kivule Ilala wakati wa kikao mkutano ulioandaliwa na DIWANI wa Kivule Nyasika Getama kuwapatia hati Wananchi wake (Katikati )Meya wa halmashauri ya Jiji OMARY KUMBILAMOTO.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akimpa Hati ya Kiwanja Mwenezi wa CCM Wilaya Ilala Mwinyimkuu Sangaraza Katika mkutano ulioandaliwa na DIWANI wa Kivule Nyasika Getama (katikati )Meya wa halmashauri ya Jiji OMARY KUMBILAMOTO.
Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kimbilamoto akizungumza na WANANCHI WA kivule katika mkutano Naibu Waziri Ridhiwani KIKWETE (Katikati)Katika mkutano ulioandaliwa na Diwani Nyasika Getama (Kushoto).
Diwani wa Kata ya Kivule Nyasika Getama akizungumza na Wananchi wake wakati Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete (Kulia )alipokuwa akikabidhi Hati