Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
SPIKA wa Bunge, na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson amechangia Sh 2 Milioni kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa daraja katika kata ya Ilomba Jijini Mbeya lililojengwa kwa nguvu za wananchi.
Dkt Tulia amesema leo Desemba 23,2022 alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa daraja hilo lililojengwa kwa nguvu za wananchi kwa thamani ya Sh 9.5 Milioni sambamba na michango ya wadau.
” Nimekuja kukagua na kuzinduliwa kwa daraja hilo ambalo wananchi wamejenga kwa nguvu zao na pia nimesikia ombi leo kwa Halmashauri ya Jijini, lakini kwa sasa wana mambo mengi sana haya kutekeleza acha mimi kama mwakilishi wenu michango shilingi Milioni mbili ” amesema. Aidha akiwa katika mkutano wa hadhara Dkt Tulia amesema Serikali imetokea zaidi ya Sh 5 bilioni kwa ajili ya kuzalisha utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa maji kutoka mgonjwa kiwira wilayani Rungwe mkoani Mbeya. ”
Wakati utekelezaji wa miradi wa maji ikiendelea na utekelezaji tayari kuna makampuni nane yameingia kwa ajili ya kuomba za zabuni ya ujenzi wa barabara njia nne kutoka uyole mpaka njia panda ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA).
Katika kuongeza nguvu na kasi ya kukamilika haraka kwa ujenzi huo, Dkt. Tulia naye amechangia Shilingi 2,000,000/ huku akiwasisitiza Wananchi hao kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama hizo.
Diwani wa Kata ya Ilomba, Toneb Chaula amempongeza jitihada zinazofanyika na Spika wa Bunge, Dkt.Tulia ikiwepo ujenzi wa miundombinu ya elimu, barabara kwa kuishawishi Serikali kutoa fedha kwa Mkoa.
Chaula amesema kuwa mpaka kufikia kujitolea kujenga daraja hilo kulikuwa na viashiria vya hatari katika daraja hili kabla ya kujengwa hasa watoto wadogo.
“Tunaomba Ofisi yako itusaidie zaidi ya hapa, tuna wadau wamejitokeza kutusaidia katika ujenzi huu ili daraja letu liwe imara zaidi ya hapa” amesema Diwani huyo.
Sophia Juma ni mkazi wa Ilomba Jijini Mbeya amesema kuwa daraja hilo lilikuwa changamoto kuvuka upande wa pili hasa kwa watoto wadogo.
“Kuna mtoto aliwahi kupoteza uhai wakati akivuka daraja hili wakati halijajengwa hivyo ambapo lilikuwa na hali mbaya iliyohatarisha maisha, hata tulipoambiwa mchango wa ujenzi wa daraja hatukuwa na kigugumizi cha kusita kuchangia sasababu athari tuliyokuwa tunapata ni kubwa “amesema Mwananchi huyo.
Amesema kuwa kazi kubwa inayofanywa na Mbunge wetu ni kubwa hivyo hatuwezi kumwangusha kwa jambo lolote la kimaendeleo.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa