Na Esther Macha,TimesMajira, Online, Chunya
HALMASHAURI ya wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya imesema kuwa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) umeleta mafanikio makubwa kwa wilaya hiyo kutokana na kusaidia watoto wanaotoka kwenye kaya za walengwa kurudi shule pamoja na wale wanaotimiza masharti ya afya , mahudhurio ya watoto klinki tofauti ya awali kabla ya mpango huo.
David Ngowo ni Mratibu wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF)wilayani Chunya mkoani Mbeya, amesema kuwa mpango huo umekuwa na mafanikio makubwa katika halmasahauri hiyo kwani umesaidia kwa kiasi kikubwa watoto wote wanaotoka kwenye kaya za walengwa wote kuhudhulia shule .
“Halmashauri ya wilaya chunya ni moja ya halmashauri zinazotekeleza mpango wa kunusuru kaya maskini mpango ulianza kutekeleza awamu ya kwanza mwaka 2015 sasa hivi tunatekeleza kipindi cha pili na nichukue fursa hii kuipongeza serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan huu mpango huu umekuwa na mafanikio makubwa sana kwa wilaya hii ,kwani wastani wa mahudhurio shuleni asilimia 98 mpaka 100 vile vile hata wale wanaotimiza masharti ya afya , mahudhurio ya watoto klink yanatia moyo , hivyo tunapongeza mpango wa TASAF kwani umesaidia hata watoto waliokuwa hawaendi shule wanaenda , mahudhurio klink”amesema Mratibu huyo.
Kwa mujibu Mratibu huyo alibainisha kuwa mpango pia umesaidia kupunguza changamoto ya umaskini katika halmashauri hiyo kwasasa kuna kaya zaidi ya 6,658 ambazo zinapokea zinapokea ruzuku za mpango wa kunusuru kaya maskini na mpango umekuwa na mafanikio makubwa kwa za walengwa kwani baadhi ya walengwa wapo kwenye nafasi nzuri kutokana na kufuga Kuku , Bata, Nguruwe,Ng’ombe mfano ukienda vijiji vya godima, Sangambi , Ikundu kuna mafanikio makubwa kwa walengwa.
Aidha Ngowo amesema kuwa mpango huo wakati unaanza katika halmashauri hiyo kitu cha kwanza ilikuwa kuwasaidia kujitambua sababu fedha zilikuwa kidogo hivyo waliwaunganisha kukaa na maafisa ugani ili walitakiwa kuanzisha miradi midogo midogo ya ufugaji ,biashara ndogo ndogo wao kama watalaam wanatakiwa kuwa karibu na maafisa ugani ili kuhakikisha wanawasaidia.
“Unajua huko nyuma walengwa walio wengi hawajui jinsi ya kutumia fursa za serikali ambazo zipo kwenye maeneo yao ambazo zinaweza kuwatoa kwenye umaskini ,kwasasa walengwa wote wapo vizuri wengi wamejenga nyumba , wameanzisha magenge ya biashara ,mpango umesaidia viongozi wa vijiji kuwa msaada kwa kuwajengea uwezo kufahamu changamoto za walengwa ushirikiano tunaopata kwa mkurugenzi ,Mkuu wa wilaya umesaidia mpango huo kuzidi kufanya vizuri “amesema Mratibu huyo .
Akizungumza na Timesmajira ,Selina Daudi mkazi kijiji cha Sangambi kata ya Sangambi wilayani Chunya amesema kuwa kabla ya kuingia kwenye mpango huo maisha yake hayakuwa mazuri lakini baada ya kuingia kwenye mpango huo na kupatiwa ruzuku alianza ufugaji wa kuku ,Nguruwe na kuanza kusomesha watoto wake .
Selina amesema mpango huo umemtoa mbali kimaisha kwani awali alikuwa akiishi kwenye nyumba ya nyasi lakini aliendelea kujishughulisha na biashara ambayo ilimpelekea kujenga nyumba ya nzuri iliyoezekwa kwa bati .
“Kupitia mpango huu wa TASAF umenipa akili imemfanya kuwa na mwelekeo ili maisha yasimshinde kwani hivi sasa nina fanya kazi za ufugaji wa kuku wa Malawi ambao wananiwesha kumudu maisha yangu na familia yangu “alisema Mlengwa huyo .
Oswimunda Mwalongo mkazi Godima kitongoji cha Majengo wilayani Chunya ni mnufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF)amesema kuwa kipindi cha nyuma maisha yake yalikuwa magumu kwasababu alikuwa hali milo mitatu kupitia Tasaf akaanza kupata uhakika wa chakula,baada ya kuanza kupika pombe na kuuza , kununua mbolea ,ufugaji ,kujenga nyumba kupitia mpango huo .
Mwalongo ametoa wito kwa walengwa wengine wanapopewa ruzuku hizo na TASAF kuzitumia vizuri kwa kuzalisha ili waweze kusonga mbele badala ya kurudi nyuma kutokana na fedha hizo kuzitumia kwa vitu vingine ambavyo havikuwa kwenye malengo yao .
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba