Na Mwandishi wetu,timesmajira
Wananchi wa wilaya ya Mbinga Vijijini wameiomba serikali kuvuta maji toka ziwa Nyasa nakusambaza kwenye vijiji ambavyo vina changamoto ya huduma ya upatikanaji maji safi na salama ilikuwezakutatua kero ya wananchi kutembea umbali wa zaidi ya km 10 kusaka maji.
Alikadhalika ,itasaidia kuwapunguzia adha wanafunzi wa kike wanaosoma bweni hasa wakiwa kwenye hedhi hivyo kuongeza ufahulu.
Ombi hilo limetolewa na Mwalimu ,Shemaya Edward wa sekondari ya Maguhu wakati wa matembezi ya km 36 yaliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la TETEA,amesema,kunahaja ya serikali kushirikiana na wadau mbalimbali kupeleka maji ya Ziwa Nyasa shule za Bweni, Taasisi mbali mbali na kwenye vijiji vya wilaya ya Mbinga ili kutatua changamoto ya maji.
Amesema,kwamuda mrefu wanafunzi hasa wa shule za bweni na wanachi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wahuduma ya maji,hali ambayo imechangia kuathirii masomo ya wanafunzii kwani wanalazimika kutumia muda mrefu kufata maji mtoni badala ya kusoma.
Naye Mratibu wa Matembezi hayo Maurus Nchimbi toka shirika lisilo la kiserikalil la LESCOTA,alisema kwakushirikiana na wafadhili waowashirika la TETEA Marekani wameandaa matembezi hayo ambapo Jumla ya wananchi 65 wametembea km 36 kutoka WilayaniMbinga Kijijiji cha Maguhu-Mbambabay Wilayani Nyasa kwa lengo la kuchangisha sh.12,000,000 ambazo zitasaidia kupeleka maji kwenye shule 5 na kukamilisha ujenzi wa maabara ya shule ya Nguzo sekondari ambayo inajengwa kwa nguvu za wananchi na inatarajiwa kuanza kuchukua wanafunzi mwezi Januari 2023 hivyo kuondoa adha ya kutembea km 18 kutafuta elimu.
Kwa Upande wake Mkurugenzii washirika la TETEA Victoria Mathew amesema,shirika hilo la kimarekani linasaidia kuchangisha fedha kupitia kwenye mitandao ambapo jumla ya sh 12. 1 milioni zimepatikana ambapo zitasaidia shule tano za Mango Primary school ,Mtekela, St.Luis na Makubika kupata matanki ya maji yenye ujazo wa lita 5000 na kupeleka vifaa vya ujenzi Nguzo sekondari .
Naye Upendo Mgimba ,Mwanafunzi shule ya sekondari Maguhu amewashukuru TETEA kwa msaada ambao wametoa kwani utasaidia kupunguza kero kubwa ambao wamekuwa wakitembea zaidi ya km 7 kwenda kufata maji mtoni maji ambayo anadai kuwa ni machafu na hayafai kwa matumizi ya Binadamu ila wanalazimika kutumia kutokana na shida.
Diwani kata ya Kambarage ,Gisberth Nchimbi,amewapongeza waratibu wa matembezi hayo ya kuhamasisha maendeleo ,ambapo kwenye shule ya Sekondari Nguzo ambayo inajengwa kwa nguvu za wananchi wameahidiwa kupewa 5,000,000 za vifaa vya ujenzi natayari wananchi wamechangia sh.70 milioni, Halmashauri sh.40 milioni hivyo amemuomba na Rais awasaidie kukamilisha shule hiyo ili wanafunzi waweze kupata elimu karibu na maeneo yao badala ya kutembea km 18.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba