November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TCRA yapongezwa mapinduzi huduma za kifedha

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Wananchi waliotembelea maonyesho ya huduma za kifedha yanayoendelea jijini Mwanza yameipongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kuleta mapinduzi katika huduma za kifedha na kuwezesha huduma hizo kupatikana kwa urahisi bila usumbufu.

Wakizungumza katika nyakati tofauti walipotembelea banda la Maonyesho la TCRA wananchi hao wamesema zamani kabla ya huduma za mawasiliano kuanzishwa upatikanaji wa huduma za kifedha ulikuwa na changamoto ikiwemo kupoteza muda, nauli kwenda kuzifuata na kutopatikana kwa taarifa za kifedha kwa haraka tofauti na sasa ambapo kila kitu kiko kiganjani.

Bw. Frederick Masanja amesema wakulima sasa wanapata huduma za kibenki wakiwa huko huko mashambani tofauti na mwanzo kwamba walilazimika kwenda mijini kufuata huduma.

Mwl. Costa Mabula amasema zamani suala la mishahara kwao ilikuwa changamoto tofauti na sasa ambapo upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya kisasa imerahisisha na kupongeza TCRA kwa kuwezesha.

Katika uwezeshaji sekta ya fedha TCRA inatoa leseni kwa makampuni yanayowekeza katika huduma za miundombinu ya mtandao ambapo hadi sasa yapo 20, makampuni ya huduma tumizi ambayo yapo 87na leseni za namba maalum za huduma ambapo huduma za kifedha zimepewa namba zinazoanzia 150

Wiki ya huduma za kifedha zinaadhinishwa jijini Mwanza katika viwanja vya rock city ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni elimu ya fedha kwa maendeleo ya watu.

Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Mabel Masasi akitoa vitabu vya machapisho mbalimbali ya huduma zinatolewa na mamlaka hiyo kwenye maonesho ya wiki ya Fedha yanayofanyika kwenye Viwanja vya Rock City Jijini Mwanza.