December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zaidi ya wanawake 7000 kunufaika na mradi wa ESP

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Zaidi ya wanawake 7000 kutoka katika wilaya 7 za nchi ya Tanzania wanatarajiwa kunufaika na mradi wa uwezeshaji kupitia ujuzi(ESP) ambapo mradi huo utagharimu Bilioni 45

Aidha mradi huo ambao unafadhiliwa na Nchi ya Canada umelenga kumsaidia mtoto wa kike

Akiongea na vyombo vya habari mapema Leo mshauri wa masuala ya jinsia ambaye pia ni mshauri wa mradi huo ,Dkt Alice Mumbi alisema kuwa mradi huo utaweza kuwasaidia watoto wa kike

Alisema kuwa mradi huo utatekelezwa katika halmashauri 7 ambazo ni Monduli,Morogoro,Kilwa,Singida,Nzega,Kasulu,Tarime,Kondoa,Njombe

“Siku ya Leo tumekutana hapa jijini Arusha lakini tunalenga kumuinua mtoto wa kike au mwanamke na tunarajia Matokeo ya mwisho ya ESP ni kuboresha kwa ushiriki wa wanawake na wasichana kiuchumi nchini Tanzania”aliongeza
Katika hatua nyingine aliongeza kuwa ndani ya mradi huo pia jumla ya wanafunzi 3200wataweza kushiriki katika shuguli za usawa wa kijinsia na uhamasishaji wa haki za binadamu,Huku jumla ya wafanyakazi 180wataweza kufunzwa ujuzi wa kiufundina ufundishwaji na kutoa noduli za usawa wa kijinsia na haki za binadamu

Awali katibu mkuu wizara ya elimu, sayansi na teknolojia wizara Francis Maiko alisema kuwa amedai kuwa kwa nchi ya Tanzania vyuo vya maendeleo ya wananchi vimekuwa taasisi za misingu za kudahili wanafunzi ba makundi ya watu waliopo pembezoni ambao wanalazimika kuacha mapema katika mfumo wa elimu kutokana na mazingira mbalimbali na wanaotaka kuendelea na elimu na mafunzo zaidi kwa njia mbadala

Alihitimisha kwa kusema kuwa hayo yote Sasa ndio yamesababisha wataalamu na wadau ambao watafanya kazi katika mradi huo kukutana kwa pamoja na wataweza kubadlishana maisha ya wanawake an kuondoa vikwazo vya ajira,kujiajiri,ba ujasirimali kwa kazi muhimu na msaada wa vyuo vya maendeleo ya wananchi Tanzania.

Naye Alain Roy ambaye ni makamu wa raisi kimataifa vyuo na taasisi kutoka nchini Canada alibainisha kuwa vyuo na taasisi za elimu inajuunia kupewa nafasi na wizara ya elimu Tanzania na kisha kufanya programu hiyo itamalizika mwaka baada ya miaka saba ingawaje imeshaanza kutekelezwa toka mwaka jana..