Na mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Suluhu Hassan Samia Suluhu Hassan amezindua matokeo ya sensa ya watu na makazi na kutangaza kuwa Tanzania ina jumla ya watu Milioni sitini na moja laki saba na elfu arobaini na moja na mia ishirini (61,741120).
Rais Samia ametangaza idadi hiyo leo Katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, na kusema kuwa kati ya Idadi hiyo ya watu Tanzania Bara ni watu 59,851,357 na Zanzibar ni watu 1,889,773.
Rais Samia amesema kuwa katika idadi hiyo ya watu, Wanawake ni Milion 31,688790 sawa na asilimia 51 na wanaume ni milioni 30,53130 sawa na asilimia 49Rais Samia amesema kuwa idadi hiyo ni Ongezeko la watu zaidi ya milioni 19 ukilinganisha na sensa ya miaka kumi iliyopita yaani 2012 ambapo kipindi hicho idadi ilikuwa milioni 44,928, 923.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini