November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Meya Kumbilamoto aongoza Wananchi Segerea kumuenzi Baba wa Taifa

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online (Ilala)

MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto ameongoza Wananchi wa Jimbo la Segerea kumuenzi Mwalimu Julius Nyerere kwa vitendo .

Meya Kumbilamoto aliongoza Wananchi hao katika ufunguzi wa Bonanza la Jimbo la Segerea la miaka 23 ya kifo Cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ,Bonanza lililoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli lililoenda sambamba na Maandamano kutoka Barakuda mpaka Segerea .

“Nimealikwa Leo kufungua bonanza la kumuenzi Baba wa Taifa Lililoandaliwa na Mbunge wetu wa Segerea katika siku ya leo kutakuwa na Michezo mbalimbali sehemu ya furaha nampongeza Mbunge Bonah pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Juma Mizungu na Vijana wake “alisema Kumbilamoto .

Kumbilamoto alisema Mwalimu Nyerere ameacha Mambo mengi yote yanatakiwa kukumbukwa ikiwemo kupiga vita umasikini na adui maradhiMeya alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi Bilioni 6.2 kwa ajili ya sekta ya Elimu aidha alisema mikakati ya Serikali kujenga vyuo vya veta Kila Wilaya na mkoa Ili Watanzania wapate Elimu na ujuzi wa kutosha.

Akizungumzia mikopo ya Serikali inayotolewa ngazi ya Halmashauri ya asilimia Kumi amewataka Wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambao wamekopa fedha hizo pia kurejesha fedha hizo za Serikali ambazo adhina riba .

Wakati huohuo alisema Serikali inajenga vituo vinane vya Afya vya kisasa Mkoani Dar es Salaam ikiwemo gholofa nne Kata ya Mchikichini fedha za Rais Samia Suluhu Hassan hivyo amewataka Wana Ilala kumunga Mkono Rais wetu katika utekelezaji wa Ilani .

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Ilala Juma Mizungu alisema Umoja wa Vijana Wilaya ya Ilala UVCCM Wanamuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Kata na Majimbo .

Mwenyekiti Juma Mizungu alisema Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Segerea na Umoja wa Vijana Wana fanya michezo Kwa pamoja katika madhimisho ya Baba wa Taifa Jimbo la Segerea ,awali umoja wa Vijana katika kuelekea madhimisho hayo walitembelea kuwaona watoto yatima na kupanda miti Kwa ajili ya kutunza Mazingira na vyanzo vya maji ni sehemu ya kazi alizokuwa akifanya Mwalimu Julius Nyerere.