January 13, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM Pugu watakiwa kufuata misingi ya Mwalimu Nyerere

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, (Ilala)

CHAMA cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala kimewataka Wana CCM wa Pugu kuyaenzi yote ya Mwalimu Julius Nyerere ikiwemo kujenga misingi ya Mwalimu Nyerere yote ambayo ameacha katika nchi ikiwemo tunu, amani na mshikamano .

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Al haj Said Sidde, wakati wa madhimisho ya miaka 23 ya kifo Cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, yalioandaliwa na Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Pugu ambapo walifanya ziara katika shule ya Sekondari Pugu aliposoma Mwalimu Julius Nyerere na kufundisha shule hiyo .

“Ninawaomba Wana CCM Kata ya Pugu muenzi yale yote mazuri ya Mwalimu Julius Nyerere Tunu ya nchi yetu ,ikiwemo Amani Umoja na kujenga Mshikamano kwa Watanzania” amesema Alhaj Sidde.

Mwenyekiti wa CCM Alhaj Sidde amesema Mwalimu Nyerere alikuwa mtu muhimu kwetu hasa kwa Taifa hili kuanza kumjua Mwalimu katika utekelezaji wa Ilani ya Chama tupambane kufuta ujinga maradhi tuondoe na umasikini Mwenyekiti Sidde aliwataka Wana CCM wa wilaya hiyo kumtumia vizuri Mwalimu Andrew Robert, anayeishi katika nyumba ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere iliyopo Pugu kwani ana mambo mengi ya kujifunza yalioacha Mwalimu Nyerere .

Aliwataka Wana CCM kumuomba Dua Rais wa Jamhuri ya MUUNGANO WA Tanzania Samia Suluhu Hassan, kwa kazi nzuri anayofanya utekelezaji wa Ilani na kujenga uchumi wa nchi .

Kwa upande wake Mwalimu Andrew Robert anayeishi katika nyumba ya Baba wa Taifa Pugu Sekondari alisema katika nyumba hiyo ya Pugu ndio Mwalimu Nyerere alikaa na kuandaa Katiba ya TANU na siasa ya kujitegemea na neno lake kubwa Mwalimu Nendeni Kajiungeni .

Mwalimu Robert aliwapongeza CCM Wilaya ya Ilala na CCM Pugu kwani Uhuru wa Tanganyika ulipatikana Ilala uwezi kuzungumza Uhuru wa Tanganyika bila kuitaja Ilala .

Makamu Mkuu wa Shule ya Pugu sekondari Ndimangwa Nzota alisema Baba wa Taifa alikuwa na hofu na Mwenyezi Mungu nchi itakuwa na Amani na mshikamano kwa kujenga UMOJA ,nguvu na mshikamano.

Ndimangwa alisema Mwalimu alipoambiwa achague kazi na kuwakomboa Watanzania Mwalimu alichagua kuwakomboa Watanzania kwanza wanyonge ,masikini Mwenyekiti wa CCM kata ya Pugu Frank MANG’ATI aliwataka Wana CCM wa Pugu na Wilaya ya Ilala kwa ujumla kujenga UMOJA na mshikamano katika kujenga Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake .

Mwenyekiti MANG’ATI alitumia nafasi hiyo kugawa mahitaji mbalimbali kwa Wanafunzi wa shule hiyo waliopo katika makundi Maalum pamoja na kufanya usafi na wanachama wa CCM Pugu mgeni rasmi akiwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Al haj Said SIDDE .

Alisema CCM Kata ya Pugu watakuwa jirani na shule hiyo na kutatua changamoto mbalimbali zilizojitokeza zikiwemo magodoro na baskeri za watu Wenye Ulemavu .