Na Ashura Jumapili, TimesMajira Online, Kagera
RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali imetenga bajeti ya sh. bilioni 100 kwa ajili ya kujenga chuo cha ufundi kila wilaya, hatua ambayo inalenga kuongeza thamani ya elimu ili kutengeneza nguvu ya Watanzania kujiajiri na kuajirika pia.
Hayo yalisemwa jana Mjini Bukoba mkoani Kagera na Rais Samia wakati akizindua Chuo kipya cha ufundi kilichojengwa kwa msaada wa watu wa China.
Aidha, Rais Samia alisema Serikali itatumia bilioni 1.1 kila mwezi kuendesha chuo hiki, ambapo malipo kwa wanafunzi yatakuwa, hivyo watamudu kujilipia.
Chuo hicho kina uwezo wa kupokea vijana 400 ambapo vijana 20 wasiokuwa na uwezo watalipiwa na Rais Samia. Kati ya vijana hao, wanawake ni 10 na wanaume 10.
“Na kukabidhiwa chuo cha ufundi kilichojengwa na watu wa China, nawashukuru Wachina kwa kuwa na msaada mkubwa katika nchi yetu nchini,” alisema Rais Samia na kuongeza kuwa Wachina waekuwa wakitoa misaada ya kubwa kwa Taifa la Tanzania.
“Ujenzi wa Chuo hiki ni sehemu muafaka kwa nchi yetu. Nawapongeza wote waliojitoa kwa dhati na kwa moyo mmoja katika kuhakikisha kazi inakamilika kwa ufanisi,”alisema.
Aliwataa Watanzania watunze majengo hayo na mashine zote zilizowekwa kwenye karakana. “Watunze majengo na mashine zilizowewa ili ziweze kuhudumia wanafunzi kwa miaka mingi zaidi,”alisema.
Alifafanua kwaba Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere Nyerere aliongoza kwa vitendo vita dhidi ya maadui watatu (aradhi ujinga na umaskini) na Serikali za Tanzania zinaendelea kupambana na maadui hawa.
Alifafanua kwamba idadi ya watu inaongezeka na kuibua mahitaji mengi kwa binadamu. “Kilichopo leo ni kufungua chuo ambacho kazi kubwa Serikali ilishafanya.
Wanafunzi jukumu lao ni kwenda kusoma elimu ya ujuzi. Na kama alivyosema waziri wa elimu, kunaongeza thamani ya elimu ili kutengeneza nguvu ya kuweza kujiajiri na kuajirika pia.
Wachina wanapaswa kushukuriwa kwa kujitolea ujenzi wa chuo hiki. Serikali itaboresha maeneo mbalimbali.”
Rais Samia aligusia pia tatizo la ukosefu wa ajira akasema ndio maana wameamua kuingia na ujenzi wa vyuo vya ufundi ili kuwezesha vijana kujiajiri na kuajirika.
“Asilimia 12 ya vijana wote wa Tanzania hawana ajira. Asilimia kubwa ni vijana kuliko watoto na wakubwa. Kazi ni kuhakikisha kuwa asilimia hiyo 12 inaongeezewa thamani kwa kuwaingiza kwenye ujuzi,” alisisitiza Rais Samia.
Alitaja hatua zingine zinazochukuliwa na Serikali kuwa ni kuendelea kuwekeza kwa vijana kwa kutengenezwa.
“Mafundi stadi pia wanahitajika kwenye miradi ya kimkkati. Vijana wenye ujuzi wanahitajika zaidi. Maeneo yote hayo ya miradi yataongeza thamani kwa vijana wa Tanzania,” alisema Rais Samia na kuongeza kwaba ndiyo aana Serikali inataka kuweka chuo kila wilaya.
Alisea vyuo vipya na vya ufundi ni vizuri na wanatambua mkakati wa dhana ya elimu ujuzi. “Watoto wa Kagera wajiunge na vyuo vya ujuzi. Wakihitimu mafunzo wajiajiri.” Alisema.
Alitoa maagizo kwa wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha vijana hao waendelezwe kwa kutengewa maeneo na kununulia sare na fursa nyingine, wahitimu wajipange vizuri.
More Stories
Tanzania Mwenyeji wa Mkutano wa nchi zinazozalisha kahawa Afrika
Watatu mbaroni kwa tuhuma za mauaji wakigombania shamba
Ng’ombe 10 wamekufa kwa kupigwa na radi