Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku nne kuanzia Oktoba 15,mwaka huu mkoani Mwanza.
Ambapo katika ziara hiyo anatarajia kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo kuzindua jengo la huduma ya macho kwenye hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando.
Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 13,mwaka huu juu ya ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima alisema Waziri Mkuu atakuwa na ziara ya siku nne yenye lengo la kutembelea,kukagua na kuzindua miradi mbalimbali.
Amesema Oktoba 16 atakagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Magufuli na baadaye kusalimia wananchi wa maeneo ya Busisi na Usagara.
Malima alieleza kuwa baada ya kusalimia wananchi hao ataelekea Bukwimba- wilayani Kwimba kukagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na baadae kuzindua jengo la huduma ya macho la Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
Oktoba 17 Majaliwa atakagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Irugwa kisha atakagua ujenzi wa shule ya Sekondari Irugwa na baada ya ukaguzi huo, ataelekea kisiwa cha Gana kukagua ujenzi wa zahanati ya Gana hatua ya msingi.
“Siku hiyo hiyo Majaliwa atarejea wilayani Nyamagana ambapo atakagua ujenzi wa stendi mpya ya Mabasi Nyegezi, na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Meli ya MV. Mwanza Hapa Kazi tu katika Bandari ya Mwanza Kusini,”amesema Malima.
Hivyo ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wa mkoani Mwanza kujitokeza kwa wingi barabarani kumpokea Waziri Mkuu kama ilivyo jadi ya wana Mwanza kuwakarimu wageni.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu