Na David John, Timesmajira Online, Mbeya
MKUU wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema pamoja na kuwa na mabadiliko ya tabia nchi lakini bado katika vipando vya Jeshi la kujenga taifa na mashamba yake kwa ujumla na vikosi yameendelea kufanya vizuri na mazao yanastawi kwa jinsi ambavyo walikuwa wametalajia.
Amesema kuwa wao walishaona changamoto hizo za mabadiliko ya tabia nchi hivyo walishaanza kufanya mawasiliano na mamlaka ya hali ya hewa ambapo walikuwa wanapewa taarifa juu ya mabadiliko hayo hususani kwenye eneo la mvua kwamba msimu huo mvua zitawahi ama kuchelewa na kama zitawahi zitakuja kwa viwango vidogo.
Amesema kuwa baada ya kupata taarifa hiyo wao kama Jeshi la kujenga taifa walikaa chinin nakuweza kujipanga na kuona aina ya mbegu ambazo zitaweza kuendana na hali ya hewa.
Brigedia Mabena ameyasema hayo Agosti 7 kwenye maonyesho ya nanenane ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Mbeya wakati alipotembelea banda la JKT pamoja na mambo mengine amesema kuwa katika kikosi cha 847 KJ ni Milundikwa nakwamba pale kikosini wamefanikiwa kwani wameweza kufikia malengo waliyokusudia.
Ameongeza kuwa baada ya kuwasiliana na mamlaka ya hali ya hewa waliweza kulima mapema ,kupanda mapema mbegu ambazo ziliweza kuhimili ukame kwa hali hiyo jeshi la kujenga taifa wakawa wamefanikiwa lakini la pili niwamba wanataka kuondokana na kilimo cha kutegemea mvua hivyo jeshi hilo limekuja na mkakati wa kilimo cha umwagiliaji wameaza katika kikosi cha 837kj ni chita tayari sikimu ya umwagiliaji imeshafikia asilimia 80 za hakeri 2500 na mpango ni kuhakikisha kwamba hekari 12000 zilizopo pale zitajengewa sikimu ya umwagiliaji.
Amefafanu kwa kufanya hivyo watakuwa wanauhaki wa kile wanachokilima na wanachokivuna na katika takwimu wanazozipata kwenye mamlaka zinaonyesha kuwa kumekuwa na uhaba wa mvua kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hivyo wao kama jeshi la kujenga taifa wanatoa rai kwa wakulima wadogo,wakulima wakati na wakulima wakubwa kuhifadhi chakula walichokipata.
“Jeshi la kujenga taifa tunahakikisha chakula tulichokipata kwa msimu huu tunaaza kwaza kuwalisha vijana wetu na kile kilichobaki ndio tunapeleka kwa jamii ili kuhakikisha tunakabiliana na hili balaa la njaa lakini hali si mbaya sana cha msingi ni kuhakikisha chakula kinachopatikana kisiuzwe nje ya nchi.”amesema Brigedia Mabena
Nakuongeza kuwa “Changamoto iliyojitokeza imeweza kutoa fursa kwao kama jeshi kuwasiliana na mamlaka ya hali ya hewa kuhakikisha kwamba wanapewa elimu kwamba msimu ujao hali itakuwaje na pili kuhakikuisha kwamba wanaaza kwenda kwenye kilimo cha umwagiliaji kwasababu nchi yetu imebalikiwa ina mito ina mabwawa,ina maziwa hivyo kuna teknolojia ambayo haitahi gharama nyingi kwani ukipata pamp na mipira kwa ajili ya umwagiliaji unaweza kumwagilia mashamba yaliyopo karibu na mito au maziwa .
Amesema kuwa jeshi hilo kwa kushirikia na taasisi zingine ikiwemo Wizara ya kilimo kwa pamoja wanahakikisha wanapata mbegu bora na wanakwenda kuongeza kilimo cha umwagiliaji na mashamba mengi yanafikiwa na yanadhalishwa kwa ubora.
“Jeshi la kujenga taifa limeaza kuboresha shamba letu la michikichi lililopo kikosi 821 kigoma kwahiyo sasahivi wanalima na wamejipanga kulima hekari 200 na kuhakikisha kwamba tunakuza hili shamba kutokana na michikichi na pia kwaupande wa zao la alizeti kule lililopo Dodoma karibu na Singida na vilevile mikoa mingine hivyo wanakuja mpango wa kuyaongeza mashamba na wanawasiliana na taasisi ya mbegu za kilimo TARI kushirikiana na watalamu waliopo katika jeshi ili kupata kitu bora.”amesema
kwa upande wake Mwenyekiti wa Maonyesho ya nanenane kitaifa JKT Kanali Shija Lupi amesema kuwa mwaka huu wanakwenda kwenye sensa ili kuangalia idadi ya watu waliopo Tanzania ambayo itachukuliwa katika mpango mzima wa kupanga mipango mizuri kwani ukingalia katika sekta ya kilimo uvuvi pamoja na shughuli zingine.
“Wito kwa watanzania nivema kushiriki zoezi la sensa ambalo linatarajia kufanya Agosti 23 ili serikali iweze kupanga vizuri shughuli za maendele hivyo nawasihi watanzania kushiriki kwani litaweza kutuvusha baada ya serikali kupanga mipango yake.”amesema Kanali Lupi.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa