November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bodi ya Chai kuondoa chai ya zamani ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo

Na Joyce Kasiki,Mbeya

MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Chai Nchini Nicolaus amesema,Bodi hiyo ,imeweka mkakati wa kuondoa asilimia 60 ya chai ya zamani hapa nchini kwenda mpya ili waweze kuongeza uzalishaji wa zao hilo  ikiwemo kuongeza mnyororo wa thamani.

Mauya ameyasema hayo katika maonyesho ya wakulima Nane Nane Jijini Mbeya wakati akizungumza na waandishi wa habariambapo amesema, moja ya mikakati waliyoweka tasnia hiyo ni pamoja na kubadili mfumo wa kilimo hicho ili wakulima waondokane na mazoea na badala yake watumie teknolojia mpya ya uzalishaji wa zao la Chai ili kupanua wigo wa soko la zao hilo hapa nchini.

Amesema, wananchi wanapaswa kuendelea kutumia chai ya Tanzania ili kusaidia kupanua wigo wa soko la zao hilo ndani na nje ya nchi ikiwemo wao wenyewe kujiinua kiuchumi na taifa kwa ujumla.

Mbali na hilo amesema jamii inapaswa kujenga mazoea ya kutumia Chai ya Tanzania kama moja ya kutangaza bidhaa zao lakini pia watachangia kwa kiasi kikubwa kuiongezea mnyororo wa thamani.

Amesema katika maonyesho hayo Tasnia ya Chai wamekuja kutoa elimu kwa jamii ili kuhakikisha wanajua na kutambua umuhimu wa Chai inayozalishwa hapa nchini pamoja na matumizi yake kwa ujumla.

“Naomba wakulima waendelee kutumia chai ya Tanzania wakifanya hivyo watasaidia kupanua wigo wa soko la bidhaa hiyo hapa ndani na nje”alisema Mauya.

Amesema muelekeo wa Tasnia ya chai hivi sasa ni pamoja na kuangalia ubora ili waweze kuzalisha vizuri,kubadili mfumo,kuongeza Pembejeo pamoja na kuongeza idadi ya uzalishaji.

Amefafanua kuwa wanafanya hivyo ili kuongeza uzalishaji wa Chai hapa nchini ikiwemo kuhakikisha Tasnia ya chai inakuwa kwa kasi hapa nchini hasa ukizingatia serikali imeongeza bajeti kwenye sekta ya kilimo.

Amesema wamejipanga kuhakikisha wanazalisha chai zaidi ya miche milion 60 ikiwemo kuongeza uchangiaji wa pato la Taifa.

MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Chai Nchini Nicolaus Mauya akionyesha kwenye ramani mikoa inayolima chai

Hata hivyo amewasisitiza watanzania kuendelea kununua chai ya Tanzania ili kuiongezea thamani.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa maendeleo ya wakulima wadogo wa chai Tanzania (TSHTDA) Theophord Ndunguru amesema moja ya mikakati waliojiwekea kama tasnia ni kuhakikisha wakulima wanatambua mbinu mbalimbali zilizoboreshwa kwenye tasnia hiyo ili waweze kuendedha kilimo cha kisasa.

Ndunguru amesema moja ya mkakati waliopanga ni kujakikisha wakulima hao wanaondokana na kilimo cha mazoea na badala yake waendeshe kilimo cha kisasa ili kuongeza idadi ya uzalishaji.

Amesema zao la chai ni la mihimu sana hivyo wakulima wanapaswa kujua teknolojia ya kisasa ya kilimo cha cha chai.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania (TSHTDA) Theophord Ndunguru (kushoto) akiwa katika shamba darasa la chai katika maonyesho ya wakulima NaneNane katika viwanja John Mwakangale Jijini Mbeya

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utafiti wa taasisi ya Chai Tanzania, Dkt. Daniel Mgori amesema ili kuongeza uzalishaji wa zao la Chai tasnia hiyo imezingatia suala la utafiti wa aina za chai inayotakowa kupandwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Amesema wao kama watafiti tayari wamegundua aina nane za miche ya Chai inayotakiwa kupandwa ili wakulima wavune kwa wingi.