Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
WATANZANIA wamesisitizwa kuendelea kufuga ikiwa ni pamoja na kuboresha mifugo yao ili kuweza kuwa na ufugaji wenye tija ambao utaweza kuwapeleka mbele zaidi wafugaji.Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Mbogo Ranches ya Mbarali Estate, Pirmohamed Mulla wakati wa akikabidhi Dume la kisasa kwa serikali kwa ajili ya uzalishaji wa Mbegu bora za mifugo.
Mulla amesema kuwa shughuli iliyowaleta ni makabidhiano ya Dume la Mbegu ambalo linakwenda wizara ya mifugo na uzalishaji uvuvi ambapo Dume hilo limepokelewa na waziri wa mifugo Mashimba Ndaki.
“Sisi kama wafugaji tumefarijika sana kwasababu Ng’ombe ambao huwa kwenye vitu kama hivyo wanapitia ukaguzi wa hali ya kwa hiyo serikali nayo ilifanya ukaguzi wake na kuridhika kwamba Dume wetu ana sifa zote za kuweza kwenda kwenye kitu cha kuzalisha Mbegu na sisi tulivyoona hivyo tuliwatembelea na kuona shughuli wanazofanya na mtambo ipo vizur”Amesema Mkurugenzi huyo.
Akielezea zaidi Mulla amesema kuwa baada ya kujiridhisha kwa pande zote mbili walifikia makubaliano na kutoa Dume huyo wa Mbegu ambapo waziri Mashimba alifurahishwa ubora wa Dume hilo.
“Dume huyu ana uwezo wa kuzalisha mbegu 150 katika uhai wake lakini watalaam katika uzalishaji wanaweza kufikia Mbegu 5000 mpaka 6000 kwa njia ya upandishaji” amesema.
Kwa upande waziri wa mifugo na Uvuvi , Mashimba Ndaki amesema Serikali imelenga kupunguza mifugo kuchungwa na kuhamasisha wafugaji kufuga mifugo ya ndani ili kupunguza migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji.
Amesema Serikali wanaliona tatizo mbele ambalo wanaweza kulikabili la upungufu wa maeneo kwa ajili ya kuchungia, kwahiyo wanashukuru kampuni ya Mbogo kwa kuwapatia dume ambalo wa naamini litatusaidia.
Hata hivyo Waziri Ndaki amewataka wadau wengine wa ufugaji kushirikiana na Serikali kupata mbegu bora za mifugo ili kuboresha hali ya ufugaji nchini na kuifanya sekta hiyo kuwa miongoni mwa sekta zinazoliingiza taifa fedha nyingi bila kuzaa migogoro.
More Stories
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato
Wambura asikitishwa na makundi CCM Nyakato