Na Iddy Lugendo, Timesmajira online Mbeya
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imesema kuwa washiriki wote katika mnyororo wa mbolea ya ruzuku lengo ni kuhakikisha wakulima wanapata mbolea katika kuwa na usalama wa chakula nchini.
Mfumo wa usajili wa mbolea wa ruzuku kwa wadau wote umejibu changamoto za wakulima kwani hakuna udanganyifu unaoweza kufanyika.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa yanayofanyika Kanda ya Mbeya Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA Dkt.Stephan Ngailo amesema kuwa katika mnyororo wa mboleo ya Ruzuku wadau wote wanatakiwa kujisajili katika mfumo ili kuondoa changamoto ya kufikia mkulima wakati wa msimu wa kilimo ukiannza.
Wadau hao wanaotakiwa kujisajili katika mfumo waagizaji wa mbolea kutoka nje ya nchi, Wazalishaji wa Mbolea nchini , Mawakala wa Mbolea nchini pamoja na wakulima ambao ndio walengwa wa mbolea ya ruzuku.
Dkt.Ngailo amesema kuwa kwa upande wa wakulima watajisajili katika ofisi za kijiji ambao watapewa namba maalum ambapo atapokwenda kwa wakala atanyesha hiyo na kununua mbolea kwa bei nafuu.
Amesema serikali imefanya hivyo katika kuwa na usalama wa chakula pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao nchini.
Dkt.Ngailo amesema TFRA imejipanga katika kusimammia mbolea ya ruzuku kwani Rais Samia Suluhu Hassan ametoa Ruzuku ya mbolea katika kuhakikisha wananchi wanapunguziwa makali ya kununua mbolea.
Aidha amesema katika maonesho ya Nane Nane Kitaifa Kanda ya Mbeya wananchi watembelee banda TFRA kupata masuala ya mbalimbali ya mbolea.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa