Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya
MAKAMU wa Rais Dkt. Philip Mpango amezindua maonyesho ya Wakulima (Nanenane) huku akimwagiza Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Triphonia Kisiga, awape nafasi wajasiriamali waende vyuoni kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana namna ya kupata mitaji na kujiajiri ili waondoe dhana ya kuajiriwa pindi watakapohitimu masomo yao.
Akizungumza wakati akitembelea mabanda kwenye maonyesho hayo yanayoendelea Kitaifa katika viwanja vya Mwakangale Jijini Mbeya,Dkt.Mpango amesema,hatua itasaidia kuwapa nguvu vijana ya kwenda kutafuta mitaji na kujiajiri pindi wanaporudi nyumbani.
“Kama inawezekana muwaruhusu hawa wajasiriamali waende vyuni wakatoe elimu kwa wananfunzi namna wajasiriamali walivyopata mitaji na walivyoanza ujasiriamali ili kuhamasisha kundi hilo kujiunga na ujasiriamali badala ya kusubiri kuajiriwa.”amesema na kuongeza kuwa
Kwa Mujimu wa Dkt.Mpango kufanya ujasiriamali nayo ni ajira inayomwezesha mtu kujipatia kipato na siyo lazima mtu afanye kazi ya kukaa ofisini huku akisema ni vyema wanafunzi waliopo vyuoni wafikirie kujiari zaidi kwa kutumia elimu wanayoipata huko vyuoni na waweze kufanya mambo makubwa ikiwemo kuchangia katika pato la Taifa
“Wajasiriamali wamekuwa wakifanya mambo makubwa kwenye sekta hii hivyo ni vyema ninyi kama jiji na baadhi ya wajasiriamali walio chini yenu mkaweka utaratibu wa kuwaruhusu kwenda kuwafundisha kundi hilo ili lipate elimu hiyo muhimu,
“Kuna vijana wengi wanafikiria kuajiriwa peke yake lakini kumbe kwenye ujasiriamali kuna ajira hivyo ni vyema wajasiriamali wakaenda kuwafundisha ili nao waweze kujiari mara baada ya kuhitimu masomo yao,”amesisitiza Dkt.Mpango
Ametumia nafasi hiyo amewapongeza banda la ufugaji Ndege mbalimbali wakiwemo Kuku na bata kutokana na uwekezaji wa mifugo hiyo walioufanya ambao unawasaidia kuwajiinua kiuchumi wao na familia zao.
“Ujasiriamali kama huo,unapaswa kufanywa na vijana wanaohitimu vyuo ili waweze kupiga hatua kwenye kuinua uchumi lakini pia kuweza kujiajiri wso wenyewe katika maeneo mbalimbali ya ujasiriamali.
Naye Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema serikali imeonyesha utayari wa kuwekeza kwenye sekta ya kilimo huku akiwasisitiza wakulima kuheshimu sekta hiyo.
“Kwa sababu ya kuwekeza katika sekta ya fedha ndio mana tumefika hapa tulipo katika sekta ya kilimo,kwa hiyo azipongza Benki zikiwemo NMB na CRDB kwa kutoa mikopo kwa wakulima yenye riba nafuu inayowawezesha kulima kwa tija.
Waziri Bashe amezungumzia kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima ikiwemo suala la lumbesa ambapo Halmashauri zimegeuza jambo hilo kama chanzo cha mapato.
“Wizara ya kilimo tumewaandikia barua kuhusu suala hilo lakini tunaona bado lipo,”alisema Bashe
Kwa upande wake Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Mbeya Straton Chilongola alisema benki hiyo ndani ya miaka mitano imetoa mikopo ya Shilingi Trilioni 1.2 kwenye sekta ya kilimo ikiwemo kwenye mazao ambayo yamepewa kipaumbele na serikali.
Aidha amesema, NMB wametii agizo la Rais la kutaka kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima ili waweze kuchukua mikopo na kujiinua kiuchumi wao na taifa kwa ujumla.
“Tutaendelea kuwa pamoja na serikali katika kuhakikisha sekta ya kilimo inasonga mbele,”amesema Chilongola
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano