Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Nishati January Makamba bado yuko kwenye ziara ya Kijiji kwa kijiji lengo ikiwa ni kukagua, Kufatilia na kutatua kero za Wananchi kwenye sekta ya Nishati.
Akiwa Kijiji cha Kilando kata ya Kilando Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa, Wananchi waliwasilisha kilio cha gharama ya Mafuta ya Petrol na Diesel ambapo Waziri Makamba amewasihi Wananchi kuendelea kuwa na imani na Serikali yao sababu bado wanaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha bei ya mafuta nchini inapungua.
Waziri Makamba amesema; “Kuhusu suala la Mafuta ni lazima tujue sisi ni Wahanga wa bei ya Mafuta Duniani, Bahati nzuri pamoja na gharama za Mafuta Duniani bado Tanzania ndio nchi inayouza mafuta kwa gharama ndogo zaidi ukilinganisha na nchi zingine za Afrika Mashariki. Tumshukuru Mh. Rais Samia bila ruzuku ya Bilioni 100 anayoitoa kila mwezi bei ya Mafuta ingekua imeongezeka 500 kwa kila lita ya Diesel na 200 kwa kila lita ya Petrol” – Waziri Makamba.
Waziri wa Nishati, January Makamba anaendelea na ziara yake ya siku 21 kupita Kijiji kwa Kijiji na sasa anaelekea mkoa wa Mbeya.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi