Na Penina Malundo, timesmajira, online
KATIBU Mtendaji wa Eneo huru la biashara Afrika, Wamkele Mene, amesema Afrika haitafanikiwa kufikia Ukombozi wa kibiashara endapo nchi hizo zake hazitakubali kuungana na kuwa na soko la pamoja ambalo lila nchi itafanya biashara na kupeleka bidhaa bila vikwazo.
Mene alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua rasmi Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) katika viwanja vya sabasaba.
Amesema bado kunahitajika nguvu kubwa ya kuleta mapinduzi ya kibiashara kwenye nchi hizo ili zizalishe bidhaa bora na kuwa huru kufanya kwenye soko la ushindani kimataifa.
“Nchi za Afrika tunahitaji kukubaliana kuwa na soko la pamoja. Si Tanzania, Kenya wala nchi yoyote itafanikiwa kupata uhuru huu kama hazitakubalina kuwa na soko la pamoja,”mesema Mene
Ametolea mfano kwamba hata ulipoingia mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 pamoja na vita vya Ukraine, uchumi wa nchi nyingi za Afrika uliyumba kwa kuwa baadhi ya bidhaa hutegemea kutoka kwenye nchi hizo.
“Na ndio maana nasema hivi hakuna mtu yeyote atakayetoka duniani huko kuja kututafutia ukombozi kwenye eneo hili, tunahitaji kushirikiana kupambana wenyewe, “amesema Mene.
Kwa Upande wa Waziri wa Viwanda na Biashara, Ashatu Kijaji, amesema wamemhakikishia kiongozi huyo wa soko huru la biashara Afrika kuwa wanatumia soko hilo kuuza bidhaa zenye ubora.
“Kiongozi huyu baada ya kutembelea mabanda yetu, amesema amegundua tunatengeneza bidhaa nzuri na bora, lakini shida kubwa iliyopo ni kwamba bado hatujafahamu namna ya kuchangamkia soko nje ya Tanzania na ametushauri tuzioongezee thamani na tukashindane,”amesema Kijaji.
More Stories
Bei za mafuta Novemba 2024,zaendelea Kushuka
TARURA yaomba Mkandarasi aitwe
Ilemela yakusanya bilioni 3.7.robo ya kwanza