Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Wakala wa vipimo Tanzania (WMA) imewataka wananchi kufanya biashara ndani na nje ya nchi kwa kufuata taratibu zote za kimataifa zinazohusu upimaji.
Hayo ameyasema Mtendaji Mkuu kutoka Wakala wa vipimo Tanzania (WMA ), Stellah Kahwa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya biashara ya 46 sabasaba
Kahwa amesema Wakala wa vipimo ni mwanachama wa shirika la vipimo Duniani hivyo wanafuata maelekezo, kanuni na taratibu za kimataifa ambazo huwa zinatolewa na shirika la vipimo Duniani.
Mbali na hayo Kahwa amesema katika maonesho hayo mbali na kuja kutangaza biashara yao lakini pia wamekuja kupata elimu na kujifunza kutoka kwa wafanyabishara wa nje;
“Tumekuja hapa kwaajili ya kuwahabarisha wananchi wetu na pia kuangalia wenzenu waliotoka nje wamekuja na nini ambapo tunaweza kujifunza kutoka kwao ili kuwa rahisi sisi kuwaelekeza wafanyabiashara wetu na wananchi kwa ujumla katika ufanyaji biashara”
Aidha amesema Katika maonesho hayo wamekuja kuonyesha kazi mbalimbali za upimaji wa vipimo kama mizani ya kidigitali, mawe yanayotumika katika mizani ya mawe, mizani yenyewe ya mawe, bima za maji, Bima za Umeme na maeneo mengine mapya.
Pia Kahwa alizungumzia juu ya muitikio mzima katika hali ya uzingatiaji vipimo nchini;”Muitikio katika hali nzima ya uzingatiaji vipimo nchini ni mzuri kwasababu watu wengi wamejifunza na bado wanaendelea kuzingatia upimaji bidhaa kwa usahihi”
Jukumu kuu la Wakala wa vipimo Tanzania (WMA) ni kuhakiki vipimo na kuhakikisha kwamba vinatumika kwa usahihi ambapo ili mfanyabiashara aweze kufanya biashara vizuri lazima awe na vipimo vilivyo sahihi na kila bidhaa inafungashwa kwa usahihi
More Stories
Rais Samia kuzindua mfuko wa kuendeleza kazi za wabunifu
Makalla ampongeza Lissu kukiri CHADEMA haina wagombea Serikali za Mitaa
Chande azindua misheni ya uangalizi uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika