Na Penina Malundo,timesmajira, Online
IMEELEZWA kuwa wazazi au walezi wanapaswa kutenga muda wao wa kukaa na watoto na kuwaeleza maana ya ukatili wa kijinsia,rushwa ya ngono pamoja na mimba za utotoni ili kuweza kuwajenga katika mazingira yaliyobora.
Hayo yamezungumzwa jana jijini Dar es Salaam,Mwanaharakati na Mwalimu wa masuala ya Jinsia,Dinah Mbaga, amesema haki ya usawa na jinsia inatakiwa kuzingatiwa kwa watoto katika kuwapatia haki zao.
Amesema kwa sasa kumekuwa na vitendo vingi vingi vinavyoendelea katika jamii ikiwemo ubakaji na vitendo vya kulawiti hivyo wazazi wakitenga siku na kuzungumza na watoto wataweza kuwasidia kwa kiasi kikubwa.
”Tutumie siku hii kuwaeleza watoto maana ya ukatili wa kijinsia na tutumie siku kama hii ya kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika katika kuelimisha watoto kuhusu ukatili,madhara wanayopata katika ukatili na viashiria vya ukatili,rushwa ya ngono na mimba za utoto,”amesema na kuongeza
”Kwa kufanya hivi tutaweza kuokoa vizazi vyetu kuondokana na madhila haya yanayoendelea ambayo kwa asilimia kubwa yanafanywa na watu wakaribu,”amesemaÂ
Kwa Upande wake Mwakilishi Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto Kituo cha Polisi Tabata ,Rajabu Phinias amesema ukatili wa kijinsia mara nyingi unatokea kipindi cha likizo ambapo watoto wengi wanakubwa na vitendo vya ubakwaji.
Amesema sababu kubwa inayofanywa kuwepo kwa vitendo hiyo ni kutokana na wazazi au walezi kuachana ama kutengana kunawafanya watoto kutolelewa katika maadili mzuri.
Naye Meneja Mipango wa Tabata Women Tapo(TAPO),Lulu Nyapili amesema taasisi yao imefanikiwa kutoa elimu ya kupinga ukatili wa dhisi ya watoto katika shule mbalimbali za msingi na sekondari zilizopo manispaa ya Ilala hususani kwa Tabata.
More Stories
Prof. Mwakalila asisitiza uadilifu, uzalendo kwa wanafunzi wapya chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Benki ya Equity Tanzania yasaini mkataba wa kuwawezesha wanawake kiuchumi
Rais Samia alivyoguswa kifo cha msanii Grace Mapunda