Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Wamaasai kutoka maeneo mbalimbali wamefanya maandamano ya amani hadi ubalozi wa Kenya Tanzania, uliopo Oysterbay jijini Dar es salaam leo juni 17, 2022 kuiomba serikali ya Kenya iingilie kati upotoshaji unaofanywa na asasi za kiraia na wanaharakati katika zoezi la kuhama kwa hiari linaloendelea katika wilaya ya ngorongoro pamoja na tarafa ya loliondo.
Wamasai hao wameeleza kuwa upotoshaji huo umelenga kuichonganisha jamii ya wamaasai na serikali ya Tanzania, pamoja na kuzorotesha jitihada mbalimbali za makubaliano zilizofikiwa na pande zote mbili.
Hayo yameelezwa kupitia barua ya pamoja iliyosainiwa na katibu wa umoja huo anayetambulika kwa jina la loishiye lashilunye iliyosomwa na kiongozi wa msafara aliyejitambulisha kwa jina moja la emanuel.
Hatua hii inakuja baada ya zoezi la kuweka alama za mipaka katika eneo la loliondo pamoja na uhamaji wa wananchi wa Ngorongoro ambapo licha ya serikali kutanabaisha uwepo wa makazi mapya katika eneo la handeni, kumetokea upotoshaji na uchochezi unaolenga kukwamisha zoezi hilo.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi